Maisha na Mafanikio : Ofisi ya Rais-Utumishi yafanya Uchaguzi kumtafuta Mfanyakazi Bora 2015 - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Friday, 24 April 2015

Maisha na Mafanikio : Ofisi ya Rais-Utumishi yafanya Uchaguzi kumtafuta Mfanyakazi Bora 2015


Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakitoa salamu ya wafanyakazi wakati wa uchaguzi wa kumpata mfanyakazi bora wa ofisi kwa mwaka 2015 uliofanyika jana katika ofisi hiyo.
Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakisikiliza maelekezo ya uchaguzi wa mfanyakazi bora wa ofisi kwa mwaka 2015 uliofanyika jana katika ofisi hiyo.
Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji wa Maadili Bw. Methew Kirama mwenye Ipad (wa kwanza kushoto) akichukua matukio wakati wa uchaguzi wa kumpata mfanyakazi bora wa ofisi ya Rais – Utumishi kwa mwaka 2015 uliofanyika jana katika ofisi hiyo.
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. HAB Mkwizu akimtangaza mfanyakazi bora wa ofisi wa mwaka 2015 mara baada ya uchaguzi kufanyika jana katika ofisi hiyo.
Mfanyakazi bora wa Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma wa mwaka 2015 Bw. Francis Sangunaa (kulia) akiwashukuru watumishi baada ya kuchaguliwa katika uchaguzi uliofanyika jana.
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. HAB Mkwizu akitoa maelekezo ya kumpata mfanyakazi bora wa ofisi kwa mwaka 2015 uliofanyika jana.

No comments:

Post a Comment