KUTOKA MEZANI KWA BALOZI, IMETOSHA FOUNDATION;
Ndugu zangu habari za jioni, najua mmechoka lakini nina machache ningependa kuwajuza.
La kwanza ni kuhusiana na uvumi ulioenea hasa katika nchi za nje, unaodai kwamba serikali imekataza watu wenye ulemavu wa ngozi kuandaa matembezi au maandamano.
Hili suala sio kweli, ili ufanye mambo kama haya ni lazima upitie taratibu za kisheria ili upate kibali. Hii ni nchi na ina taratibu zake kwa hiyo tulipaswa kuzifuata na ndio kilichosababisha hata matembezi yetu kuahirishwa. Tulikuwa tunafuata taratibu na leo rasmi tumepata usajili na leo IMETOSHA imepiga hatua kutoka MOVEMENT mpaka kuwa taasisi kamili inayoitwa IMETOSHA MOVEMENT.
Napenda kuchukua wasaa huu kuwashukuru marafiki wote wanaoniunga mkono, na kunipa moyo, msinichoke kwa sababu safari bado ni ndefu.
Baada ya taratibu kukamilika, matembezi sasa yatafanyika Tarehe 28 Machi kuanzia saa 12 Alfajiri, kutoka Leaders Club tutazunguka na kurudi hapo, karibuni sana tuchangie harakati hizi zenye lengo zuri kwa mustakabali wa Taifa letu lenye sifa ya amani na utulivu.
Nimesikia kuna wenzetu watatu wamefanya matembezi huko Mwanza na sasa wako njiani kuelekea Butiama, kwa jina hili hili la IMETOSHA. Nawashukuru kwa kutuunga mkono kwa njia hiyo ingawa wangetujulisha na sisi tungeweza kufanya jambo kuwaunga mkono au kuwasaidia chochote.
Mwisho naomba niwashukuru wote ambao mpaka sasa wanatamani kuwa sehemu ya wanafamilia, milango iko wazi, mimi napatikana kwa simu namba +255 787 000 880.
Kwa pamoja tusaidiane kupaaza sauti kupinga mauaji na unyanyapaa kwa wenzetu wenye ulemavu wa ngozi kwa kusema kwa sauti moja #IMETOSHA
AMVUNJA MBAVU MKE WAKE KWA WIVU WA MAPENZI
-
Jeshi la Polisi Mkoa wa Lindi linamsaka Hamidu Abdalah kwa kosa la
kumjeruhi kwa kumpiga na chaga ya kitanda mke wake Amina Athuman Said 40,
mkazi wa Likon...
7 hours ago
No comments:
Post a Comment