Katika mapishi ya leo ni namna ya kuunga dagaa kwa nazi na kufanya mboga iwe tamu haswaaa.
MAHITAJI
- Dagaa ( Kiasi ya kutosha watu wanne)
- Kitunguu maji kimoja
- Souse ya nyanya ( Endelea kusoma utaona maelezo juu ya hii)
- Karoti moja au mbili
- Tui moja la nazi ( Liwe tui zito)
Mimi huwa naandaa souse ya nyanya ambayo huwa inafaa kwa matumizi ya kuunga mboga mbali mbali – na ndio hiyo souse naizungumzia . Hata wewe waweza andaa na kisha ukaweka kwa friji ukawa unachukia kiasi unachohitaji wakati wa mapishi yako.
Jinsi ya kuandaa – MAHITAJI sasa hapa nitakupa kwa ujumla maana siwezi jua wewe utaandaa souse kiasi gani
- Nyanya za kutosha
- Vitunguu Maji
- Vitunguu swaumu
- mafuta ya kula ( vegetable oil)
- Binzari
- Pilipili Manga
- Mixed Herbs
- Mustard
- Chumvi
- Supu ya kuku au nyama ya ngome ( kwa wingi)
SASA TUENDELEE NA DAGAA ZETU
Andaa dagaa wako tayari kwa mapishi – Waoshe vizuri na maji moto kabisa , hakikisha hawana mchanga, wakaushe kwa jua au kwa oven – pale unapoona panakufaa.
Weka chombo katika moto kile ambacho utatumia – weka mafuta kiasi na uweke kitunguu – kitunguu kikiwa kimeiva bila kubadilika rangi weka wale dagaa wako. Endelea kuwaunga unga hapo kisha weka karoti zako hapo pamoja na ile souse yako. Ongeza maji kidogo kisha funika ichemke kwa dakika 3-4 , ili dagaa walainike kidogo na maji yapungue. Kisha weka lile tui lako la nazi; koroga kwa muda hadi liwe tayari na hii huwa ni dakika 2-3.
Sasa toa mchuzi wako wa dagaa maana hapo ni tayari na ni nzuri kula na ugali.
No comments:
Post a Comment