Mkuu
wa Habari wa BBC Idhaa ya Ulimwengu,Bi. Nikki Clarke akikata utepe
kuashiria uzinduzi rasmi wa Kituo cha kurushia Matangazo ya Idhaa ya
Kiswahili ya BBC jijini Dar es Salaam,katika Jengo lao lililopo
Mikocheni.Kushoto ni Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC, Ali Saleh.
Mkuu
wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC, Ali Saleh (wa tatu kulia) akiwapatia
maelekezo Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Dkt. Salim Ahmed Salim na Mwenyekiti
wa CUF,Prof. Ibrahim Lipumba ya namna Idhaa hiyo inavyoandaa vipindi
yake na inavyopeleka hewani wakati wa hafla ya Uzinduzi rasmi wa Kituo
cha kurushia Matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya BBC,jijini Dar es
Salaam.
Mkuu
wa Habari wa BBC Idhaa ya Ulimwengu,Bi. Nikki Clarke akibadilishana
mawazo na aliewahi kuwa Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC,Bw. Tiddo
Mhando wakati wa hafla hiyo.
Mkuu
wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC jijini Dar es Salaam,Hassan Mhelela
(kushoto) akizungumza katika hafla hiyo pamoja na kuitambulisha timu
yake.
Baadhi
ya Wageni waalikwa wakiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi wakuu wa
BBC waliokuwepo kwenye hafla hiyo,jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa zamani wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC,Bw. Tiddo Mhando (kulia) akiwa
katika mazungumzo na Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC,Bw. Ali Saleh
pamoja na Mtangazaji Sussani Mongi.
Taswira za Studio za BBC jijini Dar.
Chumba cha Habari cha BBC jijini Dar.
Wadau Salim Kikeke na Nicolas wakipitia habari kabla ya kuipeleka hewani.
BBC
Idhaa ya Ulimwengu, imezindua ofisi zake jijini Dar es Salaam. Ofisi za
Dar es Salaam zina studio ambazo zinatumika kuandaa matangazo maarufu ya
redio ya asubuhi, Amka na BBC, na pia kuendesha tovuti ya
bbcswahili.com.
Katika
kuadhimisha uzinduzi huo, vipindi vingine viwili vya BBC Idhaa ya
Kiswahili, Dira ya Dunia ya redio na ya TV vitaandaliwa kutoka Dar es
Salaam katika siku hiyo ya Jumatatu Agosti 11.
Ufunguzi
wa ofisi za Dar es Salaam ni matokeo ya mikakati ya BBC Idhaa ya
Ulimwengu ya kuhamisha uandaaji wa vipindi vya redio na tovuti kutoka
London kwenda Afrika Mashariki.
Ofisi
mpya ina vifaa vya kisasa vinavyoweza kutayarisha vipindi vya redio, TV
na huduma za habari kwa njia ya simu za mkononi. Amka na BBC, kipindi
cha nusu saa ambacho hutangazwa Jumatatu hadi Ijumaa humulika matukio na
taarifa zitakazojiri katika siku, sasa kitaandaliwa Dar es Salaam na
watayarishaji na watangazaji 15.
Ofisi
mpya pia zina watayarishaji wanaoandaa taarifa mbalimbali za kanda ya
Afrika Mashariki na Kati kwa ajili ya vipindi vya TV vya Focus on Africa
na Dira ya Dunia. Mkuu wa Habari wa BBC Idhaa ya Ulimwengu Nikki Clarke
amesema:
"Uzinduzi
wa ofisi zetu za Dar es Salaam ni hatua kubwa katika safari yetu
iliyoanza muda mrefu kidogo, katika kuwapa wanachotaka wasikilizaji
katika nchi zinazozungumza Kiswahili, na ambao husikiliza BBC wanapotaka
kupata taarifa wanazoziamini na zenye uhakika. Takriban watu milioni
12.4 - ambao ni kama nusu ya idadi ya watu wazima nchini Tanzania,
husikiliza matangazo ya redio ya BBC kila wiki.
Na
sasa moja ya kipindi maarufu cha BBC, Amka na BBC, kimekuja karibu zaidi
na wasikilizaji." Ofisi ya Dar es Salaam, ina studio mbili za redio
ambazo zinaweza kutumika na hadi watu sita kwa wakati mmoja, na hivyo ni
muafaka kabisa kwa kipindi kichangamfu cha Amka na BBC kwa ajili ya
mijadala na mahojiano ya kuvutia.
Mkuu
wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC, Ali Saleh anasema : "Ofisi mpya zinatoa
nafasi bora kabisa kwa watayarishaji wa BBC nchini Tanzania kuimarisha
ukusanyaji wa habari na kutoa taarifa kutoka katika eneo la Afrika
Mashariki na Kati.
Amka
na BBC itakuwa na uwezo mkubwa zaidi kutoa taarifa na habari
mchanganyiko, za Afrika Mashariki na pia za dunia, pamoja na mahojiano
ya moja kwa moja na watu mbalimbali, lakini pia makala na habari za
kijamii." Idhaa ya Kiswahili ya BBC imekuwa kitovu cha hatua ya BBC
Idhaa ya Ulimwengu ya kuimarisha kuwepo kwake katika sekta ya habari
barani Afrika.
Baada
ya ufunguzi wa ofisi ya Nairobi mwaka 1998, BBC Idhaa ya Ulimwengu
ilikuwa shirika la kwanza la habari la kimataifa kuwa na kituo cha
uandaaji habari barani Afrika. Mwaka 2006 Amka na BBC ilihamishwa kutoka
London kwenda Nairobi, na BBC Idhaa ya Ulimwengu, kwa mara nyingine
tena ikawa shirika la kwanza la kimataifa la habari kuandaa na kutangaza
vipindi kutoka barani Afrika.
Katika
hatua ya kuhamisha utayarisaji wa vipindi na taarifa za kwenye tovuti,
kipindi maarufu cha jioni cha redio, Dira ya Dunia sasa kinatayarishwa
Nairobi. Mwisho// Kwa taarifa zaidi wasiliana na afisa wa idara ya
mawasiliano ya BBC Idhaa ya Ulimwengu - Lala Najafova,
lala.najafova@bbc.co.uk.
Kwa
wahariri: BBC Idhaa ya Ulimwengu ni shirika la utangazaji la kimataifa
lenye idhaa nyingi za lugha mbalimbali zinazotoa huduma ya matangazo ya
redio, TV, kwenye mtandao wa internet na pia simu za mkononi. BBC Idhaa
ya Ulimwengu hutumia njia mbalimbali kuwafikia wasikilizaji wake wapatao
milioni 191 duniani kote. BBC huwafikia watu milioni 265 duniani kote
kila wiki kwa huduma zake kutoka BBC Idhaa ya Ulimwengu, BBC News TV na
bbc.com.
No comments:
Post a Comment