Waziri
wa Viwanda na Biashara Dkt. Abdalah Kigoda na Balozi wa China Nchini
Dkt. Lu Youqing wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa maonyesho ya siku
nne ya bidhaa zinazotengenezwa nchini China.
Mtendaji
Mkuu wa kampuni ya Shenzhen Yingli New Energy Resources Honglin Hui
(Kulia) akimueleza Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Abdalah Kigoda
(kushoto) jinsi Solar Panel inayotengenezwa na kampuni hiyo inavyofanya
kazi wakati wa maonyesho ya bidhaa zinazotengenezwa nchini China
yaliyofunguliwa leo katika ukumbi wa Diamond Jubilee uliopo jijini Dar
es Salaam.
Waziri
wa Viwanda na Biashara Dkt. Abdalah Kigoda akiangalia pikipiki aina ya
SWAN inayotengenezwa na kampuni ya Honda ambayo inayotumia mafuta ya
Petrol na Umeme wakati wa maonyesho ya bidhaa zinazotengenezwa nchini
China. Kulia kwake ni Balozi wa China nchini Dkt. Lu Youqing na kushoto
ni Juwes Wang ambaye ni mfanyakazi wa kampuni hiyo.
Waziri
wa Viwanda na Biashara Dkt. Abdalah Kigoda akiangalia viatu
vinavyozalishwa nchini China wakati wa maonyesho ya siku nne ya bidhaa
zinazotengenezwa nchini humo ambayo yamefunguliwa leo na kumalizika
jumapili ya tarehe 24/8/2014.
Waziri
wa Viwanda na Biashara Dkt. Abdalah Kigoda akiangalia vitenge
vinavyozalishwa nchini China wakati wa maonyesho ya siku nne ya bidhaa
zinazotengenezwa nchini humo .
Balozi
wa China Nchini Dkt. Lu Youqing akimkabidhi zawadi Waziri wa Viwanda na
Biashara Dkt. Abdalah Kigoda wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya bidhaa
zinazotengenezwa nchini humo.
Charley
Peng kutoka kampuni ya China Wuxi Everbright akimwonyesha Waziri wa
Viwanda na Biashara Dkt. Abdalah Kigoda bajaji aina ya Dudu
inayozalishwa na kampuni hiyo.
Waziri
wa Viwanda na Biashara Dkt. Abdalah Kigoda akimsikiliza Balozi wa China
Nchini Dkt. Lu Youqing wakati wa hafla fupi ya ufunguzi wa maonyesho ya
bidhaa zinazotengenezwa nchini humo.
Baadhi
ya wageni aliohudhuria sherehe za ufunguzi wa maonyesho ya siku nne ya
bidhaa zinazotengenezwa nchini China wakimsikiliza Waziri wa Viwanda
na Biashara Dkt. Abdalah Kigoda (hayupo pichani) .
Picha na Anna Nkinda- Maelezo
No comments:
Post a Comment