Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais
Mazingira, Dk. Mhandisi Binilith Mahenge (mwenye
shati la drafti) akipiga picha maji yanayopita kwenye
mto Kibandu kutoka kiwanda cha NIDA Textile
Mills Ltd.Kulia ni Diwani wa Kata ya Kigogo
Richard Chengula.
Bustani ya mchicha ikiwa pembeni mwa mto
Kibangu ambayo hutumia maji yanayotoka kwenye
kiwanda cha NIDA.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais
Mazingira, Dk. Mhandisi Binilith Mahenge (kulia)
akipiga picha bomba linalotiririsha maji machafu
kutoka kiwanda cha NIDA.
Bomba linalotoa maji machafu kutoka kiwanda cha
NIDA.
Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi ya
Mazingira (NEMC) Bonaventure Baya (anayeonesha
kidole) akimueleza jambo Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais Mazingira, Dk. Mhandisi Binilith
Mahenge, juu ya maji yanayotoka kwenye kiwanda
cha NIDA.Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara
hiyo Mhandisi Angelina Madete.
Afisa Tawala wa kiwanda hicho Mohamed Honelo
(kulia) akiwakaribisha Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais Mazingira, Dk. Mhandisi Binilith
Mahenge na Naibu katibu Mkuu wa Wizara hiyo
Mhandisi Angelina Madete, walipowasili kiwandani
hapo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais
Mazingira, Dk. Mhandisi Binilith Mahenge (katikati)
akiongozwa na Meneja Mkuu wa NIDA Textile
Mills Ltd Imran Lohya kupanda kwenye tenki la maji
yanayutumika na kiwanda hicho.
Maji hayo yanavyoonekana.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais
Mazingira, Dk. Mhandisi Binilith Mahenge,
akizungumza na wana habari baada ya ziara.
Afisa Tawala wa kiwanda hicho Mohamed
Honelo akiwaeleza wana habari kuhusu hali
iliyoshuhudiwa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais
Mazingira, Dk. Mhandisi Binilith Mahenge,akitoa
maelezo ya mwisho kabla ya kuondoka kiwandani
hapo.
Picha zote na Hussein Makame -MAELEZO
Na Winner Abraham-MAELEZO
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira,
Dk. Mhandisi Binilith Mahenge ametoa onyo kwa
kiwanda cha NIDA Textile Mills Ltd, kutokana na
kutititirisha maji yasiyo salama kwa mazingira na afya ya
wakazi wa eneo la kiwanda hicho.
Waziri Mahenge alitoa onyo hilo wakati alipotembelea
kukagua kiwanda hicho kilichopo Kigogo Mkuyuni jijini
Dar es Salaam, baada ya kupata taarifa kuwa kiwanda
hicho kinatiririsha maji machafu yanayoathiri mazingira.
Awali kiwanda hicho kiliomba cheti cha usafi wa
mazingira kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi ya Mazingira
(NEMC) na Waziri huyo aliombwa kutia saini cheti hicho
ili kuthibitisha usafi wa kiwanda hicho.
Hata hivyo, Wazari Dk Mahenge alikuwa akipokea
malalamiko kutoka kwa wananchi juu ya NIDA
kukiuka taratibu za usafi kwa kutiririsha maji machafu
yanayowaathiri wananchi.
Waziri pamoja na timu yake akiwemo Mkurugenzi
Mkuu wa NEMC, alifanya ukaguzi wa kustukiza kwenye
kiwanda hicho na kukuta kikitiririsha maji yasiyo salama
kwenye mto Kibangu unaopita maeneo mbalimbali ya jiji
la Dar es Salaam.
Hata hivyo, baada ya Waziri na timu yake kuingia
kiwandani hapo, walitembelea maeneo mbalimbali ya
kiwanda hicho na baadaye aliutaka uongozi wa kiwanda
hicho kwenda kujionea maji machafu yanayotoka
kiwandani humo.
Kwa mshangao mkubwa, Waziri pamoja na timu yake
walikuta maji yaliyokuwa yakitiririshwa ni tofauti na yale
waliyoyashuhudia awali wakati walipokagua kabla.
“La kwanza ambalo ninataka Watanzania walifahamu ni
kwamba tunataka sana wawekezaji na Serikali imeweka
mazingira mazuri sana kuvutia wawekezaji, lakini
mwekezaji mzuri atakuwa ni yule tu anayejali mazingira”
alisema Waziri Dk. Mahenge na kuongeza:
“Ukiona kinachofanyika hapa ni kama vile mwekezaji
anajali cha kwake hajali maisha ya Watanzania....mimi
kwangu nimepewa malalamiko ofisini karibu mara nne,
tulipita mara kwanza na sasa tumeona haya, maana
yake ni kama wenzetu hawa wanaidanganya sekta ya
uwekezaji”
Alisema kuwa walidhani ili wapate ushirikiano mzuri ni
lazima wajali mazingira ya mto huo hutumiwa kupandwa
mbogamboga, watoto wadogo wanavuka humo, hivyo
wakipata kemikali hizo watapata madhara makubwa sana.
“Maji tuliyoyakuta asubuhi sio haya ambayo mmeenda
kuyafungua sasa hivi, maana yake mitambo nyinyi
mnayo isipokuwa ama kwa gharama zenu mnazoogopa
au umeme au nini hamfungulii, vilevile mnaonekana
hamuwajali Watanzania” alisema Waziri Dk. Mahenge.
Alibainisha kuwa kwa mtindo huo hawawezi kupewa
cheti cha usafi wa mazingira kama hatapata uhakika
kwamba maji yataendelea kuwa mazuri kwa muda
wote huku akinoesha hofu kuwa iwapo watapewa cheti
wataendelea kudanganya Watanzania.
Afisa Tawala wa kiwanda hicho Mohamed Honelo
aliahidi kuwa watafanya marekebisho na kuweka
mazingira katika hali ya usafi kwa muda wote na kuomba
radhi kwa Serikali kutokana na hali hiyo.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Bonaventure
Baya alisema wanajipanga kuhakikisha kuwa
wanaweka utaratibu wa kuhakikisha kuwa kiwanda hicho
kinazingatia masharti ya usafi wa mazingira kwa muda
wote.
No comments:
Post a Comment