Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Balozi wa Oman nchini Tanzania, Saoud
Ali Mohammed Al-Ruqaish, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es
Salaam, leo Julai 3, 2014 kwa mazungumzo.
Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Oman nchini Tanzania,
Saoud Ali Mohammed Al-Ruqaish, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar
es Salaam, leo kwa mazungumzo.
Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Balozi wa Syria nchini Tanzania, Abdulmonem
Annan, wakati alipofika Ofisini kwake
Ikulu jijini Dar es Salaam, leo kwa mazungumzo.
Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Syria nchini Tanzania, Abdulmonem
Annan, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo kwa mazungumzo.
********************************************
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
AKUTANA NA MABALOZI WA OMAN NA SYRIA
Ikulu
jijini Dar es Salaam, Julai 03, 2014
Makamu
wa Rais wa Jmahuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mohammed Gharib Bilal leo
Alhamisi Julai 03, 2014 amekutana na Waheshimiwa Mabalozi wa nchi za Oman na
Syria wanaowakilisha nchi zao hapa Tanzania. Mheshimiwa Makamu wa Rais
amekutana na Mabalozi hao ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam.
Awali
alikuwa ni Balozi wa Oman, Mheshimiwa Saoud Ali Mohammed Al-Ruqaish aliyefika
kukutana na Mheshimiwa Makamu na kufafanua kuwa uhusiano baina ya Tanzania na
Oman unazidi kuimarika na kwamba wawekezaji kutoka Oman wamekuwa wakija kwa
wingi kuwekeza Tanzania tofauti na siku za nyuma huku pia Tanzania ikionesha
kufungua milango yake kwa uwekezaji mkubwa wa kati nchini Tanzania.
Kwa
upande wa Balozi wa Syria Mheshimiwa Abdulmonem Annan yeye alimueleza
Mheshimiwa Makamu wa Rais kuwa Syria iko katika kipindi kigumu na kwamba nchi
hiyo kwa sasa inatafuta kila linalowezekana kurejesha amani. Balozi huyo
alifafanua kuwa nchi yake inahitaji msaada wa nchi za Kimataifa ili kusaidia
kuweka pande zote zinazokinzana mezani kwa lengo la kufikia maazimio
yatakayoifanya nchi hiyo isiparanganyike.
Mheshimiwa
Makamu wa Rais alimueleza Balozi za Syria kuwa, Tanzania inatamani sana kuona
hali ya utulivu inarejea Syria na kwamba nchi hiyo inaendelea kujenga uchumi
uliobomoka tayari. Pia alisema kuwa msimamo wa Tanzania unabakia katika kutaka
pande zinazohusika katika mgogoro huo zinafuikia suluhu kwa amani ili wananchi
wengi wasipoteze maisha.
Imetolewa na: Ofisi ya Makamu wa Rais
Ikulu Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment