Baadhi
ya Akina Mama wa Kijiji cha Mvuleni Kidoti wakitoka ndani ya pango
kujipatia huduma za maji safi wakishuhudiwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya
Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Balozi Seif aliyetembelea kijiji hicho.
Katibu
wa CCM Tawi la Nungwi Nd. Adibu Ali Sheha akitoa Taarifa fupi ya
Maskani ya CCM ya Amani na Utulivu ya Kijiji hicho ambayo itajengwa kwa
mchanga wa Makamu Mwenyekiti wa CCM, Zanzibar Dr. Ali Mohd Sheni kwa
kushirikiana na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali
Iddi.
Baadhi
ya wanamaskani ya amani na Utulivu ya Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja
wakisikilizika Majumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Balozi Seif hayupo
pichani aliyefika kwenye maskani hiyo kutekeleza ahadi waliyotoa na Rais
wa Zanzibar Dr. Ali Mohd Sheni.
Mjumbe
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi
akizungumza na Wanamaskani ya Amani na Utulivu Nungwi Mkoa wa Kaskazini
Unguja.
Balozi
Seif akimkabidhi fedha Taslim Shilingi Milioni 4,000,000/- Mwanachama
wa Maskani ya Amani na Utulivu ya Nungwi Bibi Leila Kheir Haji kwa ajili
ya ujenzi wa maskani yao ikiwa ni utekelezaji wa ahadi waliyoitoa na
Rais wa Zanzibar.
Baadhi
ya Akina Mama wa Kijiji cha Mvuleni Kidoti wakitoka ndani ya pango
kujipatia huduma za maji safi wakishuhudiwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya
Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Balozi Seif aliyetembelea kijiji hicho.
Balozi
Seif akikagua Msikiti wa Ijumaa wa Kijiji cha Mvuleni ambao unahitajika
kunyanyuliwa ili kutoa hufrsa nzuri kwa waumini wa dini ya Kiislamu
kufanya ibadaza yao kwa utulivu.
Balozi
Seif akikagua Msikiti wa Ijumaa wa Kijiji cha Mvuleni ambao unahitajika
kunyanyuliwa ili kutoa fursa nzuri kwa waumini wa dini ya Kiislamu
kufanya ibadaza yao kwa utulivu.Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
***************************************
Mjumbe
wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi Balozi
Seif Ali Iddi amewathibitishia Wana CCM, Wananchi na Jamii kwamba
ataendelea kufuatilia matatizo na changa moto zinazowakabili wananchi
popote pale akiwa kama mtendaji Mkuu wa Serikali.
Alisema
Wanasiasa wasifikirie kwamba anapokwenda majimboni hasa katika maeneo
yanayoongozwa na Upinzani wakadhani ya kuwa anakwenda kuvuruga siasa za
vyama vyengine vya upinzani.
Balozi
Seif alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na Wana Maskani ya CCM ya
Amani na Utulivu iliyopo katika Kijiji cha Nungwi Mkoa wa Kaskazini
Unguja akitekeleza ahadi waliyoitoa yeye na Makamu Mwenyekiti wa CCM
Zanzibar Dr. Ali Moh’d Sheni katika ziara yao ya Tarehe 2 Mei Mwaka
2013 ya kujenga Maskani hiyo katika hadhi ya kisasa.
Akikabidhi
mchango wa shilingi Milioni 4,000,000/- zitakazotumika katika ujenzi wa
Maskani hiyo Balozi Seif alisema bado ana wajibu wa kufanya hivyo kwa
vile yeye ni kiongozi wa Serikali na Siasa.
Alifahamisha
kwamba anachokifanya muda wote ni kuangalia shida na kero
zinazowakabili Wananchi na kutafuta mbinu za kuzikwamua na zile zilizo
nje ya uwezo wake huziwasilisha Serikalini kwa hatua zaidi ya kutafutiwa
ufumbuzi muwafaka.
Aliwashangaa
baadhi ya viongozi wa kisiasa wanaoendelea kumshutumu kwa kitendo na
uamuzi wake wa kufuatilia kero, matatizo na changamoto hizo
zinazowakabili wana jamii katika maeneo yao mbali mbali hapa Nchini.
“
Hivi nikuulizeni Wananchi, ni kweli hamuhitaji huduma za maji
zinazoletwa na Serikali ? Kweli hamuhitaji hudum za umeme
zinazotengenezewa miundo mbinu na Serikali ambazo baadhi ya wanasiasa
zinawakera ? “ Aliuliza Balozi Seif.
Mjumbe
huyo wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM ambae pia ni
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwaomba wananchi wasibabaishwe na
maneno ya wanasiasa wasiowatakia maendeleo yao.
Mapema
akitoa Taarifa fupi ya wana Maskani hao wa CCM wa Amani na Utulivu ya
Nungwi Katibu wa Tawi la CCM la Kijiji hicho Nd. Adibu Ali Sheha alisema
wana maskani hao wamepiga hatua kubwa katika utekelezaji wa Ilani na
Sera za CCM tokea kuanzishwa kwake.
Ndu.
Adibu alisema licha ya utekelezaji huo wa sera za CCM lakini wana
Maskani hao wapatao 85 hivi sasa pia huendesha miradi ya kujiongezea
mapato kwa kujishughulisha na kazi za mikono ikiwemo ushonaji wa mikoba,
mikeka makawa na charahani.
Hata
hivyo Nd. Adibu alieleza kwamba wana maskani hao wanakabiliwa na tatizo
la ukosefu wa mashine ya kudarzi ili kufanikisha kazi zao tatizo ambalo
Balozi Seif alilichukuwa na kuahidi kulifanya kazi.
Baadaye
Balozi Seif alipata fursa ya kukagua pango kubwa la maji liliopo katika
Kijiji cha Mvuleni ambalo Wananchi wa Kijiji hicho hulitumia kwa kupata
huduma za maji licha ya kwamba baadhi ya msimu maji hayo huchaganyika
na maji ya chumvi kutegemea kima cha maji ya bahari .
Balozi
Seif alishuhudia changamoto kubwa inayowapata wananchi hao hasa akina
mama ya kusaka huduma hiyo muhimu kwa kulazimika kuteremka na kupanda
mlima mkubwa uliopo pembezoni mwa pango hilo.
Balozi
Seif pia aliangalia jengo la Msikiti wa Ijumaa wa Kijiji cha Mvuleni na
kuwaagiza waumini wa Msikiti huo kumtafuta fundi atakayefanya tathmini
ya makisio ya kujengwa upya kwa paa, vyoo na sehemu ya nyongeza ya nje
ili kuwapa utulivu wa ibada waumini hao.
Akizungumza
na Wananchi hao mara baada ya ziara hiyo fupi Balozi Seif
aliwahakikishia kwamba Wahandisi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar wanajiandaa
kuliondosha tatizo la huduma za maji safi katika Kijiji hicho.
Alisema
wahandishi hao wamethibitisha kwamba huduma za maji safi na salama
zinatarajiwa kupatikana ndani ya Kijiji hicho katika kipindi cha miezi
mitatu kupitia kisima cha maji kiliopo Kigongoni.
Aliwaeleza
wananachi hao kwamba Mamlaka ya Maji Zanzibar haijapuuza wazo lao la
kuchimbiwa kisima chao ndani ya Kijiji hicho, lakini kinachohofiwa na
wataalamu hao ni mazingira ya maji katika eneo hilo ambayo baadhi ya
wakati huchanganyika na maji ya chumvi.
Katika
kuunga mkono juhudi za Mamlaka ya Maji Zanzibar za kuwapatia maji safi
na salama wananchi hao wa Kijiji cha Mvuleni Balozi Seif aliahidi
kuchangia shilingi Milioni 5,000,000/- zitakazoongeza nguvu za
utekelezaji wa kazi hiyo.
Naye
Mke wa Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM
Mama Asha Suleiman Iddi aliwatanabahisha akina mama wa Vijiji hivyo
kujiepusha na ushawishi wa vurugu za wanasiasa ambazo hatma yake huzaa
matatizo yasiyokwisha.
Mama
Asha alisema dunia imekuwa ikiendelea kushuhudia madhila na maafa
yanayowapata wanawake na watoto hasa katika maeneo yanayozunguukwa na
migogo ya kisiasa pamoja na vita.
Mapema
Balozi Seif alikabidhi Fedha Taslimu shilingi Milioni 1,600,000/- kwa
Vikundi vya Hiari ya Moyo, Hatuyumbi Maskani, Vijana wa Dufu pamoja na
Vijana wa CCM wa kijiji hicho waliopatiwa pia sare za CCM ambapo kila
kikundikatika mgao huo kimepata shilingi Laki 400,000/-.
Balozi
Seif pia akakabidhi Futari, mashafu, Juzuu kwa wananchi wa Kijiji cha
Mvuleni pamoja na Seti ya Jezi kwa timu ya Vijana wa Chama cha Mapinduzi
wa Kijiji hicho.
No comments:
Post a Comment