Mkurugenzi wa Takwimu za Kijamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS),
Morice Oyuke (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa
habari mjini Morogoro leo wakati akifungua Warsha ya siku moja ya
kuwajengea uwezo wanahabari kuhusu namna bora ya kuandika habari za
kitakwimu. Kulia ni Meneja wa Takwimu za Pato la Taifa, Daniel Masolwa.
Mkurugenzi
wa Takwimu za Kijamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Morice Oyuke
(kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini
Morogoro leo wakati akifungua Warsha ya siku moja ya kuwajengea uwezo
wanahabari kuhusu namna bora ya kuandika habari za kitakwimu. Kulia ni
Meneja wa Takwimu za Pato la Taifa, Daniel Masolwa.
Mtakwimu, Stephano Cosmas, akitoa mada katika warsha hiyo.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye warsha hiyo.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye warsha hiyo.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye warsha hiyo
Wanahabari wakiwa katika warsha hiyo.
Dotto Mwaibale, Morogoro
WAANDISHI wa Habari nchini wametakiwa kutumia taaluma yao kwa ajili ya kuhamasisha Umma kuhusu umuhimu wa Takwimu.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Takwimu za Kiuchumi Morice Oyuke kwa
niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina
Chuwa.mjini Morogoro leo asubuhi wakati akifungua Warsha ya siku moja ya
kuwajengea uwezo wanahabari kuhusu namna bora ya kuandika habari za
kitakwimu.
"Ninyi
wanahabari ni muhimu katika masuala ya takwimu hivyo ni vizuri mjifunze
jinsi takwimu zinavyoisaidia serikali, wadau wa maendeleo na wadau wa
takwimu katika kupanga Sera na kufanya tathmini ya utekelezaji wa
mipango mbalimbali ya kitaifa na kimataifa kama vile Dira ya Taifa ya
Maendeleo ya mwaka 2025 Tanzania Bara na mwaka 2020 Tanzania Zanzibar"
alisema Oyuke.
Oyuke
alitaja mambo mengine wanayopaswa kujifunza ni Mkakati wa Kukuza
Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania Bara (Mkukuta) Mkakati wa Kukuza
Uchumi na Kupunguza Umaskini Zanzibar (Mkuza) na Mpango wa Taifa wa
Maendeleo wa Miaka Mitano 2010/11 mpaka 2015/16 na Malengo ya Melenia
(MDGs)
Alisema
eneo jingine watakalofundishwa ni kuhusu Pato la Taifa na jinsi
linavyokokotolewa na bei za ajira, takwimu za jamii na umuhimu wake.
Dk.Chuwa
alisema vyombo vya habari vinajukumu la kutoa taarifa sahihi zilizo
rasmi ambazo zinazalishwa na tafiti mbalimbali nchini ili ziwafikie
wadau wote nchini bila ya kupoteza maana.
No comments:
Post a Comment