A: OFISI YA WAZIRI MKUU TAMISEMI INATANGAZA ORODHA YA WANACHUO WAHITIMU WA MAFUNZO YA UALIMU KAMA IFUATAVYO:-
i. Walimu wa Cheti (Daraja IIIA) kwa ajili ya shule za msingi 17,928
ii. Walimu wa Stashahada kwa ajili ya shule za sekondari 5,416
iii. Walimu wa Shahada kwa ajili ya shule za sekondari 12,677
Walimu hawa wamepangwa katika Halmashauri na shule za mazoezi za vyuo vya ualimu Tanzania Bara.
B: Kila Mwalimu (ajira mpya) atatakiwa kuzingatia yafuatayo:-
- Kuripoti tarehe 01/04/2014 kwenye ofisi za Wakurugenzi wa Halmashauri kwa ajili ya kupangiwa vituo vya kazi na kuanza kazi.
- Mwalimu atatakiwa kuwa na vyeti vyake halisi vya chuo na Sekondari
- Walimu ambao ni waajiriwa wa Serikali waliokuwa wanajiendeleza kielimu wanatakiwa kurudi kwa waajiri wao ili kuendelea na kazi
- Fedha za kujikimu za siku saba (7) na nauli kwa walimu wapya zimetumwa katika Halmashauri walikopangwa walimu. Hivyo, kila mmoja aripoti katika Halmashauri aliyopangwa
- Mwalimu ambaye hataripoti ifikapo tarehe 10/04/2014 hatapokelewa tena na atakuwa amepoteza ajira yake.
- AJIRA MPYA YA WALIMU WAPYA KWA AJILI YA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI MWAKA 2013/14
- BOFYA HAPA KUPATA WAALIMU WA SHAHADA WALIOPANGWA SHULE ZA SEKONDARI
- BOFYA HAPA KWA WAALIMU WA STASHAHADA
- BOFYA HAPA KUPATA HABARI ZOTE ZA AJIRA YA WAALIMU WA DARAJA(III A) , STASHAHADA NA SHAHADA : NA WAALIMU WA SHAHADA WALIOPANGWA VYUONI
No comments:
Post a Comment