Mhe. Kairuki |
Naibu
Waziri wa Sheria na Katiba Mhe. Angela Jasmine Kairuki (37) ametajwa
katika jarida la kimataifa la Forbes kuwa ni mmoja wanawake vijana 20
wenye nguvu barani Afrika mwaka huu.
Katika
toleo lake la hivi karibuni chini ya kichwa cha habari ‘The 20 Young
Power Women in Africa 2013’, jarida la Forbes linamuorodhesha Mhe
Kairuki sambamba na wanawake wengine 19 kama vijana wa kike wenye nguvu
kwa nafasi zao kikazi na kibiashara.
Kutajwa
kwa Mhe Kairuki katika orodha hiyo kumezua msisimko katika mawasiliano
ya mtandao wa 'twitter' ambapo Watanzania wengi wamekuwa wakielezea
furaha na fahari zao kwa kuona Mtanzania mwenzao, tena mwanamke kijana,
anatambulika kimataifa kwa utendaji wake.
Mhe. Angela Kairuki akitembelea Jeshi la Magereza katika mojawapo ya shughuli zake za kikazi |
Wanawake
wengine waliotajwa na jarida hilo ni Mimi Alemayehou (Ethiopia) Makamu
wa RAis Mtendaji wa Overseas Private Investment Corporation (OPIC),
Vera Songwe(Cameroon) Mkurugenzi Mkazi World Bank Senegal, na Tara
Fela-Durotoye (Nigeria) Mwanzilishi wa House Of Tara.
Wengine
ni Rapelang Rabana (Afrika Kusini) Mjasiriamali, Claire Akamanzi
(Rwanda) Afisa Mtendaji Mkuu wa Rwanda Development Board, Valentina
da Luz Guebuza (Msumbiji) Mwekezaji, Hadeel Ibrahim (Sudan) wa Mo
Ibrahim Foundation, Alengot Oromait (Uganda) Mbunge, na Monica
Musonda, (Zambia) Afisa Mtendaji Mkuu na MWanzilishi wa kampuni ya Java
Foods.
Wengine
ni NoViolet Bulawayo (Zimbabwe) Mtunzi wa vitabu, Minoush Abdel-Meguid
(Misri) Mwekezaji, mjasiriamali na mwendesha benki, Ola Orekunrin
(Nigeria) Daktari na Mwanzilishi wa The Flying Doctors, Sibongile
Sambo (Afrika Kusini) Afisa Mtendaji Mkuu na Mwanzilishi wa SRS
Aviation, Lupita Nyong’o (Kenya) Mwigizaji na mtengeneza filamu,
Amini Kajunju (Congo DRC) Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa
Africa-America Institute na Folake Folarin-Coker (Nigeria) Mbunifu wa
mitindo.
Wengine
katika orodha hiyoni Lindiwe Mazibuko (Afrika Kusini) Mwanasia na
Kiongozi wa chama cha Democratic Alliance (DA) bungeni, Minoush
Abdel-Meguid (Misri) Mwekezaji, Mjasiriamali na mwendesha benki,
Sibongile Sambo (Afrika Kusini), Wangechi Mutu, (Kenya) Msanii na
mchongaji.
No comments:
Post a Comment