UKATILI KWA BINADAMU : ALIYEKUWA MWENYEKITI WA CCM MWANZA, NA DIWANI WA KATA YA KISESA BW. CLEMENT MABINA AUWAWA KWA KUPIGWA MAWE - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Monday, 16 December 2013

UKATILI KWA BINADAMU : ALIYEKUWA MWENYEKITI WA CCM MWANZA, NA DIWANI WA KATA YA KISESA BW. CLEMENT MABINA AUWAWA KWA KUPIGWA MAWE

Aliyekuwa Mwenyekiti CCM wa mkoa wa Mwanza na Diwani wa Kata ya Kisesa, Mhe. Clement Mabina enzi za uhai wake
---
 Aliyekuwa Mwenyekiti CCM wa mkoa wa Mwanza na Diwani wa Kata ya Kisesa, Mhe. Clement Mabina  ameuwawa na wananchi wenye hasira kwa kupigwa na mawe na silaha za jadi mwendo wa saa saba mchana.

Imeelezwa kuwa sababu ya kumwuua Mabina inatokana na ugomvi wa ardhi ambapo kesi ya eneo hilo ilikuwa ikiendelea mahakamani, lakini mchana wa leo, marehemu Mabina alionekana akipanda miti na kuweka mawe ya msingi katika eneo lenye ugomvi na wananchi walipomhoji kuhusu kibali cha mahakama cha kufanya hivyo, inaripotiwa kuwa aliwatolea lugha chafu na kuwatisha kwa bunduki ambapo alifyatua risasi.

Inaripotiwa kuwa risasi moja ilimuua mwananchi na alipoishiwa risasi, wananchi walimvamia kwa silaha mbalimbali ikiwemo mawe na mapanga hadi kumsababishia mauti. Kwa picha zaidi bofya hapa >>>

No comments:

Post a Comment