Rais
Jakaya Kikwete, akizungumza na wachezaji wa timu ya Taifa, Taifa Stars
jana Ikulu jijini Dar es salaam, alipokutana nao na kuwapa hamasa
waweze kupata ushindi katika mchezo wao dhidi ya Moroco utakaochezwa
Juni 7, na michezo mingine ikiwa ni hatua ya kuiwezesha timu hiyo kukata
tiketi ya kushiriki mashindano ya kombe la dunia mwaka 2014.
Meneja
wa Timu ya Taifa Stars, Tasso Mukebezi, akiteta jambo na Nahodha wa
Timu ya Taifa Stars, Juma Kaseja, Ikulu jijini Dar es salaam
walipokutana na Rais Jakaya Kikwete jana mchana.
Rais
Jakaya Kikwete akiwaaga wachezaji wa Timu ya Taifa Stars Nadir Haroub
'Canavaro' baada ya kukutana nao jana Ikulu Jijini Dar es salaam na
kuwahamasisha washinde mchezo dhidi ya timu ya Taifa ya Moroco
utakaochezwa Juni 7 mwaka huu, ikiwa ni sehemu ya Taifa Stars kutafuta
ticketi ya kucheza mashindano ya Kombe la Dunia.
Rais
Jakaya Kikwete akiwa katika Picha ya Pamoja na wachezaji wa Timu ya
Taifa , Taifa Stars, viongozi wa Wizara ya Habari, Vijana ,Utamaduni na
Michezo na Viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Rais
Jakaya Kikwete akiwa katika Picha ya Pamoja na wachezaji wa Timu ya
Taifa , Taifa Stars, viongozi wa Wizara ya Habari, Vijana ,Utamaduni na
Michezo na Viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
---
Na. Veronica Kazimoto na Aron Msigwa–MAELEZO.
Rais wa
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete jana
amekutana na timu ya Taifa (Taifa stars) kwa lengo la kuitia moyo katika
mechi ijayo kati yake na timu ya Moroco ikiwa ni harakati za Tanzania
kutafuta tiketi ya kucheza fainali za kombe la Dunia kwa mara ya kwanza
mwaka 2014.
Rais Kikwete
ameiambia timu hiyo kuwa ina uwezo mkubwa wa kusonga mbele kutokana na
uwezo mkubwa waliouonesha katika mchezo wao dhidi ya Gambia ambapo
walifanikiwa kupata ushindi wa bao 2-0.
“Maadamu
mara ya kwanza mliwashinda Gambia, hakikisheni pia mnapata ushindi dhidi
ya Moroco, mkishinda tunafurahi sana na mkishindwa tunanyong’onyea
sana,” amesema Rais Kikwete.
Aidha
amempongeza kocha wa timu hiyo Kim Poulsen pamoja na Kamati ya Taifa ya
ushindi ya Taifa stars kwa kuisaidia timu hiyo kiasi cha shilingi
milioni 30 ikiwa ni mkakati wa kuiongezea nguvu kwa hatua iliyofikia na
kuwataka wachezaji kujituma ili kuwafurahisha watanzania ambao hivi sasa
wanaipenda timu yao ya Taifa.
Nae Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Fenera Mukangara amesema
Serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa michezo nchini
ili kuondoa changamoto zinazoikabili timu hiyo.
Kwa upande
wake Kocha Poulsen, amemshukuru Rais Kikwete kwa kuwakaribisha na
kuwatia moyo ambapo ameahidi kuifundisha vizuri timu hiyo ili
kuhakikisha kuwa wanapata ushindi.
Akizungumza
kwa niaba ya wachezaji wenzake kaptaini wa timu hiyo Juma Kaseja
amemshukuru Rais Kikwete na kuahidi kujituma kwenye mazoezi na hatimaye
kuibuka washindi kwenye mechi zijazo.
Taifa stars ambayo inakamata nafasi ya pili katika kundi C inatarajia kucheza ugenini na Morocco mnamo Juni 7 mwaka huu
No comments:
Post a Comment