Dr. ALI MOHAMED SHEIN ASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA SHERIA ZANZIBAR - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Saturday, 9 February 2013

Dr. ALI MOHAMED SHEIN ASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA SHERIA ZANZIBAR

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) akifuatana na Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu,(kushoto) na Kaimu Waziri wa Katiba na Sheria pia Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Nassor Ahmed Mazrui,alipowasilin katika viwanja vya Victoria Garden,katika Maadhimisho ya  Siku ya Sheria Zanzibar,zilizofanyika juzi
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akionesha jarida la Mahakama baada ya kulizindua wakati wa sherehe za maadhimisho ya kilele cha Siku ya Sheria Zanzibar,zilizofanyika jana,katika viwanja vya Victoria garden Mjini Zanzibar,(kushoto), Kaimu  Waziri wa Katiba na Sheria,pia Biashara Viwanda na Masoko Nassor Ahmed Mazrui,na (kulia) Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na Wananchi na wanasheria  wakati wa sherehe za maadhimisho ya kilele cha Siku ya Sheria Zanzibar,zilizofanyika jana,katika viwanja vya Victoria garden Mjini Zanzibar,(kushoto), Kaimu  Waziri wa Katiba na Sheria,pia Biashara Viwanda na Masoko Nassor Ahmed Mazrui,na (kulia) Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu. 
 Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar Ibrahim Mzee,alipokuwa akizungumza wakati wa sherehe za maadhimisho ya kilele cha Siku ya Sheria Zanzibar,zilizofanyika juzi,katika viwanja vya Victoria garden Mjini Zanzibar,ambapo ujumbe wa mwaka huu unasema “Kutokomeza Unyanyasaji Kijinsia”
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(wa tatu kushoto) Jaji Kiongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano Fakih Jundu,(kutoka kushoto) na Kaimu Waziri wa Katiba na Sheria,pia Biashara Viwanda na Masoko Nassor Ahmed Mazrui,(kutoka kulia) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi khamis,Spika wa baraza la Wawakilishi Pandu Ameir Kificho na Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu,wakiangalia Kikundi cha wasanii cha Black Roots kilipokua kikitumbuiza katika kilele cha Siku ya Sheria juzi
 Viongozi wa Dini mbali mbali na Majaji wa Mkoa wakisikiliza kwa makini hotuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,aliyoitoa jana katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Sheria Zanzibar,katika Uwanja wa bustani ya Victoria Garden.
Viongozi wakisimama wakati wimbo wa Taifa wa Zanzibar ukipigwa na Brass band kikosi cha polisi katika sherehe za maadhimisho ya Siku ya Sheria Zanzibar.mara alipowasili Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiwa ndio mgeni rasmi katika hafla hiyo,iliyofanyika viwanja vya Victoria garden Mjini Unguja.Picha na Ramadhan Othman,Ikulu-Zanzibar

No comments:

Post a Comment