Askofu wa kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania dayosisi ya kaskazini kati Askofu Thomas
laizer amefariki Dunia jioni ya tarehe 7/2/2013.
Habari ambazo zimethibitishwa na katibu Mkuu wa dayosisi
hiyo Israel Ole Karyongi zimesema kuwa askofu alikumbwa na mauti majira ya
saa 12 za jioni.
“Ni kweli baba Askofu amepita na tuko katika hali ya dharura
ngumu na tungependa mtuachie nafasi ili tuwape taarifa juu ya msiba huu
kesho”alisema Karyongi akizungumza kwa njia ya simu .
Askofu laizer ndiye
askofu wa kwanza wa na mwanzilishi wa dayosisi hiyo ambayo awali ilikuwa ikiitwa dayosisi
Mkoani Arusha kabla ya mwaka juzi kubadilishwa jina na kuitwa dayosisi ya
kaskazini kati.
Ni msiba mkubwa mno katika Mkoa wa Arusha kutokana na askofu
huyo kupata umaarufu katika kazi zake za
kiroho na kijamii husasan jamii ya kabila la wamaasai.
Anatajwa kushiriki katika kuendeleza jamii hiyo kielimu kwa
kubuni na kuanzisha shule zaidi ya ishirini za sekondari zikiwemo maalum kwa
ajili ya watoto wa kike. kwa habari zaidi: bofya hapa>>>
No comments:
Post a Comment