Sajuki enzi za uhai wake
Simon Mwakifwamba (kushoto) na
wadau wengine wakimsaidia Sajuki (katikati) kutoka jukwaani baada ya
kudondoka katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha mwishoni mwa
mwaka jana.
-
Msanii maarufu wa Filamu nchini Juma Kilowoko(Sajuki)ambaye
hivi karibuni Serikali ilijitolea kubeba jukumu la kugharamia matibabu
yake na hatimaye hivi karibuni kulazwa kwenye kitengo cha wagonjwa
mahututi (ICU) kwenye hospitali ya Taifa ya Muhimbili amefariki dunia
leo Alfajiri akiwa amelazwa katika hospitali ya Muhimbili.
Mchakato wa mazishi ya Sajuki unafanyika Tabata, jijini Dar es Salaam. MUNGU ailaze ROHO ya marehemu SAJUKI mahali pema PEPONI. Ameen
Sajuki
aalifikishwa hospitalini hapo mwishoni mwa Desemba 2012, alikofikishwa akitokea
Amana, alikokuwa akipata matibabu mbaada ya kuanguka jukwaani jijini Arusha,
alipopanda kutaka kusalimia mashabiki wake ikiwa ni harakati za kutafuta fedha michango
ya pesa za kumpeleka tena India
kupata matibabu.
Katibu
wa Baraza la Filamu Tanzania
(TAFF), Wilson Makubi, amethibitisha kutokea kwa msiba wa Sajuki, ambaye alikuwa
akisubiriwa apate nafuu ili Serikali ya Tanzania
igharamie safari na matibabu yake nchini India.
Makubi
alisema kuwa, maandalizi ya msiba huo yatatangazwa baada ya wahusika na wadau
kukukutana, huku akiwataka mashabiki wa sanaa na msanii huyo kwa ujumla kuwa
wavumilivu katika kipindi hiki cha maandalizi ya mazishio yake.
Kabla
na baada ya kuifika India
kwa matibabu, Sajuki aligunduliwa kuwa na ugonjwa wa uvimbe pembeni ya ini,
ambapo aliporejea alionekana kuimarika kiafya, kabla ya kuanza kuugua tena.
Kifo
cha Sajuki kinafanya muendelezo wa vifo vya wasanii nguli wa filamu na muziki
ulioanzia mwaka uliopita, ambapo wakali kama Steven Kanumba, John Maganga,
Mlopelo, Sharo Milionea, Mariam Khamis ‘Paka Mapepe’ walifariki kwa nyakati
tofauti kutokana na maradhi na ajali.
Mchakato wa mazishi ya Sajuki unafanyika Tabata, jijini Dar es Salaam. MUNGU ailaze ROHO ya marehemu SAJUKI mahali pema PEPONI. Ameen
No comments:
Post a Comment