MH. LOWASSA AFANYA SHEREHE YA KUUKARIBISHA MWAKA MPYA 2013 MONDULI. - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Friday, 4 January 2013

MH. LOWASSA AFANYA SHEREHE YA KUUKARIBISHA MWAKA MPYA 2013 MONDULI.


Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa na Mkewe Mama Regina Lowassa wakiwapungua mikono wageni waalikwa wakati wa hafla ya Chakula cha Mchana aliyoiandaa kwa ajili ya kusherehekea Mwaka Mpya wa 2013,iliyofanyika nyumbani kwake Monduli.
Mbunge wa Jimbo la Kilindi,Mh. Beatrice Shelukindo (wa pili kulia) akiambatana na Mbunge wa Jimbo la Bariadi,Mh. Andrew Chenge wakati wakiwasili kwenye hafla ya Chakula cha Mchana iliyokuwa imeandaliwa na Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa kwa ajili ya kuukaribisha Mwaka Mpya wa 2013.
Wafanyabiashara maarufu jijini Arusha,Papa King (Mwenye TRIPLE A RADIO NA UKUMBI )na Mdau Mathias (MNEC) wakiwasili kwenye hafla hiyo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akihutubia wageni mbali mbali waliohudhulia hafla ya Chakula cha Mchana aliyoiandaa kwa ajili ya kuukaribisha Mwaka Mpya wa 2013,iliyofanyika nyumbani kwake,Monduli.

No comments:

Post a Comment