Waziri
wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa
akizungumza na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa mpango kabambe wa
Teknohama katika Sekta ya Elimu nchini uliofadhiliwa na Kampuni ya
HUAWEI kutoka China leo.
Katika
Mradi huo wa Teknohama itayowezesha Watanzania mbalimbali kutoka shule
za Sekondari na Vyuoni kupata vifaa na mafunzo ya Sayansi na Teknolojia
ili kusukuma mbele maendeleo katika nyanja za Uchumi na Kijamii.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya HUAWEI kutoka China Bw. Bruce Zhang
akizungumza katika hafla hiyo kwamba Mpango huu unaoitwa “Huawei ICT
Star” itasaidia katika shule za Primary na Sekondari katika kusukuma
mbele maendeleo ya Sayansi na Teknolojia nchini Tanzania.
Alisema
katika Program hii itasaidia kuboresha miundo mbinu katika Sanyansi na
Teknolojia ili kutoa mwamko kwa vijana wa Kitanzania kujifunza masomo ya
Sayansi na Teknolojia.
Balozi wa China nchini Tanzania Mh. LU YOUQING akitoa maelezo yake
wakati wa uzinduzi wa mpango wa Teknohama katika shule na vyuo nchini
Tanzania.
Balozi
alisema mpango huu ni mwendelezo wa uhusiano mwema kati ya Tanzania na
Jamhuri ya watu wa China katika nyanja mbalimbali za biashara uchumi na
Kijamii.
Aliongeza
kwamba Serikali ya China itaendelea na mikakati yake ya kusaidia nchi
ya Tanzania ili kuweza kufikia malengo ya Milenia ya 2015.
Meza Kuu.
Mgeni rasmi Mh. Mbarawa na Balozi wa China wakizindua rasmi mpango wa “HUAWEI ICT STAR” nchini Tanzania.
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Mbarawa na
Mkurugenzi Mtendaji wa HUAWEI Bw. Bruce Zhang wakitiliana saini kitabu
cha makubaliano rasmi ya Ushirikiano katika Sekta ya Sayansi na
Teknolojia kupitia Elimu.
Profesa Mbarawa akimkabidhi zawadi kwa Mkurugenzi Mtendaji wa HUAWEI.
Pichani Juu na Chini ni wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi huo.
Mgeni rasmi Waziri Mbarawa akiondoka ukumbi baada ya uzinduzi. Na Full shangwe Blog
No comments:
Post a Comment