DCI Robert Manumba ataja majina ya Watuhumiwa 10 walioshiriki kumuua Liberatus Barlow - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0676 643 633

Saturday, 27 October 2012

DCI Robert Manumba ataja majina ya Watuhumiwa 10 walioshiriki kumuua Liberatus Barlow


  Akitaja majina hayo mbele ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania IGP Said Mwema, MKURUGENZI wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), Robert Manumba,  amesema kuwa simu iliyoporwa ya mwanamama ambaye alikuwa akisindikizwa nyumbani na marehemu ndiyo imesaidia kukamilisha upelelezi huo hatimaye wahusika kukamatwa...
 Msikilize kwa kubofya hapa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania IGP Said Mwema akizungumzia juu ya source ya mauaji..

Baadhi ya Polisi wakifuatilia kinachojiri ndani ya ukumbi wa Halmashauri ya jiji la Mwanza jioni ya jana.Picha na Habari na Mdau Gsengo

---- 

JESHI la Polisi limewataja watuhumiwa 10, na bado linaendelea kuwatafuta watuhumiwa wengine, ambao inadai walishiriki kumuua aliyekuwa Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow.






Kati ya watu hao watano wametiwa mbaroni Mwanza  na watu watano kutoka Dar es Salaam. Leo (jana) mjini Mwanza, mbele ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania IGP Said Mwema, Mkurugenzi wa makosa ya Jinai Nchini (DCI) Robert Manumba aliwataja watuhumiwa  hao ni Muganizi Michael Peter (36) mkazi wa Isamilo ambaye inadaiwa alikiri mwenyewe kumuua kamanda kwa risasi.


Wengine ni Chacha Waitara Mwita (50), Magige Mwita Marwa, Bugazi Edward Kusota na Bhoke Mara Mwita (42) ambao walikamatwa jijini Dar es Salaam baada ya kuwekewa mtego kwa msaada wa wananchi.



Wanaoshikiliwa jijini Mwanza kwa mahojiano ni pamoja na Mwalimu Doroth Moses Lyimo aliyekuwa na RPC wakati mauaji yakitokea, Felix Felician Minde (50), Philemon Felician (46) maarufu kama Fumo, Bahati Agustino Lazaro (28) na Amos Magoto (30) maarufu kama Bonge.

 
Wengine katika orodha hiyo ni  Bahati Agustino Lazaro kabila Muha Mfanyabiashara mkazi wa Nyakabungo na Amos Weibe Magoto (Bonge) ambaye ndiye aliyekutwa na simu ya mwalimu Doroth 




Manumba amesema simu iliyoporwa ya mwanamama ambaye alikuwa akisindikizwa nyumbani na marehemu, ndiyo imesaidia kukamilisha upelelezi huo na hatimaye wahusika kukamatwa.





Alisema Kikosi kazi cha upelelezi kilichokuwa chini yake  Manumba kilijigawa kwenye makundi matatu moja ni lile la Ukamataji, Mahojiano na lingine la interejensia huku wakitumia njia ya sanyansi kwa kufuatia mitandao ya simu.




Marehemu Kamanda Barlow aliuawa  usiku wa Oktoba 12 majira ya kati ya saa 7 na 8 usiku katika eneo la Mianzi Mitatu, Kitangiri, kona ya Bwiru baada ya kupigwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi, wakati alipopita kumsindikiza Mwalimu Dorothy Moses nyumbani kwake kutoka katika kikao cha harusi kilichofanyika Mtaa wa Rufiji.

No comments:

Post a Comment