Dr. Jakaya Kikwete Akiwa ziarani nchini Kenya - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Wednesday, 12 September 2012

Dr. Jakaya Kikwete Akiwa ziarani nchini Kenya

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akipongezwa na Rais wa kenya Mwai Kibaki Muda mfupi baada ya kumaliza  kuongeana wanahabari na kisha kupiga picha ya pamoja baada ya  Mazungumzo yao Rasmi ya Kiserikali kati ya nchi hizo mbili.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akipiga picha ya pamoja na Rais wa kenya Mwai Kibaki na Viongozi wengine.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Mwai E. Kibaki wa Kenya pamoja na ujumbe wake wakiingia Ikulu ya Nairobi  Jumanne, 11 Septemba , 2012,  alipoanza Ziara Rasmi ya Kiserikali (State Visit) ya siku tatu nchini humo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete  pamoja na ujumbe wake na wenyeji wao wakianza  Mazungumzo Rasmi ya Kiserikali kati ya nchi hizo mbili.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete  akipokewa na Waziri wa Elimu ya Juu wa Kenya, Mheshimiwa Margaret Kamar alipowasili Chuo Kikuu cha Kenyatta kufungua rasmi Jengo la Shule ya Ukarimu na Utalii ya Chuo hicho.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kufungua rasmi Jengo la Shule ya Ukarimu na Utalii ya Chuo Kikuu cha Kenyatta. Kulia kwake ni Waziri wa Elimu ya Juu, Mheshimiwa Margaret Kamar  na kuhsoto kwake ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Olive Mugendi.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba ya  kufungua rasmi Jengo la Shule ya Ukarimu na Utalii ya Chuo Kikuu cha Kenyatta.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akitembezwa kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanywa na wanafunzi baada ya  kufungua rasmi Jengo la Shule ya Ukarimu na Utalii ya Chuo Kikuu cha Kenyatta.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akikabidhiwa zawadi ya picha ya kuchora baada ya  kufungua rasmi Jengo la Shule ya Ukarimu na Utalii ya Chuo Kikuu cha Kenyatta. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akipozi na wanafunzi wawili waliotoa burudani ya vichekesho wakati wa sherehe za ufunguzi rasmi wa Jengo la Shule ya Ukarimu na Utalii ya Chuo Kikuu cha Kenyatta.
Picha na IKULU

No comments:

Post a Comment