Mahakama na vyombo vya sheria vya Marekani ndio vinaongoza, kwa kuwasilisha maombi 5,950.
Asilimia 93 ya maombi hayo yalikubaliwa. Mengi yalikuwa kuhusu uchunguzi wa uhalifu.
Kampuni ya usafirishaji watalii anga za mbali Virgin Galactic itasafirisha abiria wake kwa kwanza mwaka 2013.
Taarifa hizi zimekuja wiki moja baada ya mkurugenzi wa kampuni hiyo Richard Branson kuzindua kiwanja cha kupaa na kutua cha vyombo vya anga za mbali kwenye jangwa la New Mexico.
Msemaji wa Virgin amesema haiwezi kuwa na tarehe kamili kwa sababu usalama ni kipaumbele kwao.
NetFlix, kampuni ya kwenye mtandao inayokodisha DVD za filamu imetangaza kufikisha shughuli zake Ulaya.
Kuanzia mwaka ujao, kampuni hiyo itatoa huduma zake Uingereza na Ireland.
Tovuti hiyo ndio kampuni pekee Marekani inayotoa huduma kama hiyo, lakini imepoteza wateja laki nane hivi karibuni kutokana na kuongezeka kwa bei.
Wahandisi wa zamani wa kampuni ya Apple waliotengeneza iPod wanapeleka nguvu zao kutengeneza vifaa vya nyumbani.
Ubunifu wa hivi karibuni ni kuunda kirekebisha joto hiki.
Kifaa hiki kinabadili hali ya joto na baridi kutokana na watu waliopo na jinsi wanavyotaka.
Watengenezaji wanasema unaweza kuendesha kifaa hicho kiuzwacho dola 249 kwa mbali kwa kutumia simu au hata kompyuta.
No comments:
Post a Comment