Mamlaka ya udhibiti katika sekta ya nishati na maji (EWURA) imeagiza kampuni kubwa nne za kuuza mafuta ambazo zimedaiwa kuwa vinara wa mgomo wa kuuza mafuta nchini, kuanza kuuza bidhaa hiyo mara moja ambapo pia imetoa onyo kali kwa kampuni zinazoendelea na mgomo huo. Kampuni zilizotakiwa kurejesha huduma ni BP, Engen, Camel pamoja na Oil Com. Kampuni hizo pia zimetakiwa kujieleza ndani ya saa 24 kwa nini zisichukuliwe hatua za kisheria kwa kuvuruga ugavi wa nishati ya mafuta nchini. Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Bw Haruna Masebu, amesema katika mkutano na waandishi wa habari kuwa kwa mujibu wa sheria ya uanzishwaji wa EWURA, agizo hilo ni sawa na agizo la Mahakama Kuu ya Tanzania. “Agizo hilo pia linawataka kutojihusisha na matendo yeyote ambayo yatavuruga mwenendo wa ugavi wa mafuta katika soko,” Bw Masebu alisema katika mkutano huo na waandishi wa habari. Maagizo hayo ya EWURA yanafuatia mkutano wa wajumbe wa bodi ya wakurugenzi wa mamlaka hiyo uliofanyika jana jijini Dar es Salaam kujadili hali ya mgomo wa mafuta.
KATIBU MKUU UTUMISHI AHIMIZA VIONGOZI WA UMMA KUZINGATIA UADILIFU WAKATI WA
UJAZAJI FOMU ZA TAMKO LA RASILIMALI NA MADENI
-
*Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma
Mkomi akizungumza wakati wa mafunzo ya ujazaji wa fomu za Tamko la
Rasilimali na Ma...
1 hour ago
No comments:
Post a Comment