Rais
mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi akiwatunuku
wahitimu wa kozi mbalimbali katika mahafali ya Chuo Kikuu cha Kampala
cha jijini Dar es Salaam kwenye sherehe za mahafali.
Baadhi ya waadhiri wa chuo hicho wakiwa kwenye mahafali hayo.
Rais
mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi (kushoto) na
mgeni rasmi katika mahafali ya Chuo Kikuu cha Kampala cha jijini Dar es
Salaam akiteta jambo na Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Muhammad
Ndaula katika mahafali hayo yaliyofanyika jana.
Baadhi ya wahitimu wa ngazi ya digree kozi ya afya wakila kiapo cha kuhitimu fani hiyo.
Sehemu ya wahitimu wakiwa katika mahafali hayo.
Sehemu ya wahitimu wakiwa katika mahafali hayo.
Sehemu ya wakufunzi na wahitimu wa Chuo Kikuu cha Kampala wakiwa kwenye mahafali.
Mahafali yakiendelea
Msafara wa mahafali ukiongozwa na Rais msaafu wa Awamu ya Pili, Mwinyi mara baada ya sherehe za mahafali ya nne ya Chuo Kikuu cha Kampala (KIU) cha jijini Dar es Salaam.kumalizika. |
RAIS
mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi amewataka
wahitimu wa vyuo vikuu nchini kuacha tabia ya kuchagua kazi za kufanya
mara baada ya kuhitimu elimu yao. Mwinyi alisema tabia hiyo imepitwa cha
wakati hasa katika dunia ya sasa yenye changamoto kubwa ya ajira.
Rais
Mwinyi alitoa kauli hiyo juzi wakati akizungumza na wahitimu wa
kozi mbalimbali kwenye sherehe za mahafali ya nne ya Chuo Kikuu cha
Kampala (KIU) cha jijini Dar es Salaam.
Alisema kitendo cha baadhi ya wahitimu hasa wa vyuo vikuu kupendelea kuchagua kazi za kufanya kimekuwa kikiwapotezea muda na fursa anuai, hivyo kuwataka kuacha tabia hiyo ambayo kwa kipindi hiki imepitwa na wakati.Alisema wahitimu hawana budi kuanza kufanya kazi zozote zinazojitokeza mbele yao na kutumia fursa hiyo kuelekea kwenye mafanikio kadri walivyojipangia katika maisha yao.
"...Nawapongeza wahitimu kwa hatua hii, sasa mnaingia katika maisha mapya na ya vitendo msiende kuchagua kazi za kufanya, anza na kazi yoyote inayojitokeza mbele yako kisha uitumie kutimiza ndoto zako," alisema katika hotuba yake kwa wahitimu hao.
Aidha Rais huyo mstaafu aliwataka wahitimu hao kuwa wachapakazi, wabunifu na kutumia ipasavyo ujuzi na elimu waliopewa katika ngazi mbalimbali ili kuweza kuisaidia jamii na taifa kwa ujumla.
Alisema kuwa Serikali ya Tanzania imejipanga kuhakikisha wanafunzi wote wenye sifa na vigezo vya kujiunga na chuo wanapata nafasi hiyo bila vikwazo kupitia Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu nchini (HESLB).
Akihimiza matumizi ya lugha ya Kiswahili hasa kufundisha programu katika vyuo vikuu, Mwinyi alivitaka vyuo vikuu kuanza kufundisha programu za lugha hiyo ili kuchochea matumizi yake kama yanavyofanya mataifa mengine kwenye vyuo vyao iwemo China, Urusi, USA, Iran na mengineyo.
Alisema
Afrika lazima iwe na lugha moja ya kuwaunganisha watu wake na lugha
pekee inayozungumzwa na mataifa mengi ya Afrika ni Kiswahili hivyo kuna
kila sababu ya kujivunia lugha hiyo na kuitumia ipasavyo. "...Naahidi
katika mahafali yajayo nitatoa hotuba yangu kwa lugha ya Kiswahili na
salamu zangu zote nitazitoa kwa kiswahili," alisema Mwinyi.
Awali akizungumza katika mahafali hayo, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kampala (KIU), Profesa Ndaula Muhammad alisema jumla ya wahitimu 1079 wamehitimu masomo yao katika ngazi ya Shahada, Stashahada na Asatashahada katika fani mbalimbali.