Maisha : Wananchi Watakiwa kutumia Nishati ya Biogas ili Kurahisisha Maisha - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


19 Jul 2017

Maisha : Wananchi Watakiwa kutumia Nishati ya Biogas ili Kurahisisha Maisha



Mkufunzi wa semina ya wadau mbalimbali wanaotumia Teknologia ya biogas ,pamoja na wamiliki wa mitambo hiyo pamoja na mafundi Rowah Spear akiendelea kutoa elimu katika semina hiyo inayofanyika leo jiji hapa

wakwanza kulia ni Mratibu wa Ubunifu kutoka ECHO Harold Msanya akiwa anafafanua jambo mbele ya wakufunzi hao

baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakiendelea kufanya kazi ya majadiliano katika makundi


Mkufunzi wa semina ya wadau mbalimbali wanaotumia Teknologia ya biogas ndugu Rowah Spear akiwa anawaelekeza baadhi ya wadau waliouthuria semina jinsi biogas inaweza kufanya kazi

wadau wakiendelea kufatilia mada ilikuwa inaendelea




Mkurugenzi wa ECHO Erwin Kinsey akiwa anaonyesha wakulima na wadau walioshiriki semina hiyo mmea aina ya gugukaroti ambalo ,alisema kuwa gugu ilo kwa asilimia 90% huku asilimia 10% ni gugu ambalo linaweza kutumika kutengeneza biogas(na woinde shizza,Arusha)

wadau wakiendelea na majadiliano katika makundi yao ikiwa ni sehemu ya kujifunza njia mbalimbali na matumizi ya biogas
Habari picha na Woinde Shizza,Arusha .


Wananchi wametakiwa kutumia Gesi Bayogesi kwani inapunguza gharama za watumiaji wa vyanzo vingine vya nishati ,pia gesi hii inasaida kutunza mazingira .

Hayo yamebainishwa leo na Mratibu wa Ubunifu kutoka ECHO Harold
Msanya wakati akitoa mada katika semina ya wadau mbalimbali wanaotumia Teknologia ya biogas , wamiliki wa mitambo hiyo pamoja na mafundi wanaofunga na kutengeneza mitambo hiyo .

Alisema kuwa gharama za nishati ya umeme na gesi asilia ni ghali sana hasa kwa mtumiaji atakayedhamiria kutumia jiko la umeme au jiko la gesi lakini kwa gesi hii ya samadi mtumiaji au mabaki ya nyasi aina mbalimbali zitamgharimu muda wake tu kujaza samadi na maji kila siku na atakuwa
hana malipo ya pesa kila mwezi kama itakavyomlazimu kulipia umeme na gesi asilia kila mwezi, na hata kuni ambazo watumiaji wengine hununua

Alibainisha kuwa njia hii imeweza kuwasaidia na kuwapa
faida baadhi ya wananchi ambao wameanza kutumia teknoligia hii na pia wengi wao wameshanufaika na huduma hii .

Aidha Bayogesi ambayo aghalabu hutokana na kinyesi cha wanyama, masalia ya mimea na kinyesi cha binadamu inaweza kuzalishwa na kutumika kupikia na hata matumizi mengine kama vile kuendeshea
mitambo mbalimbali.

“ Matumizi ya gesi hii kwa mtu ambaye ana mifugo kama vile nguruwe, ng’ombe yanaweza kusaidia kuondokana na gharama za kununua nishati ya kuni, mkaa, umeme na hata gesi asilia inayochimbwa ardhini.”alisema
Msanya .

Kwa upande wake mkufunzi wa Mkufunzi wa semina ya wadau mbalimbali wanaotumia Teknologia ya biogas ,pamoja na wamiliki wa mitambo hiyo pamoja na mafundi Rowah Spear alisemak uwa ni wajibu wa kila mtanzania kuwakikisha anakuwa na mtambo huo kwani mtambo huo unapunguza gharama ubwa ambazo awali walikuwa wanatumia ,na pia pale mwananchi anapotumia mtambo huu anakuwa rafiki wa mazingira kwani kwanza kabisa akati miti ovyo na pili yale majani ,vyakula ,na uchafu uchafu wa aina wowote anaweza kuukusanya na kuingiza katika mashina na
ikamsaidia kupatikana kwa Biogas.


Pia alisema kuwa mbali na kupata nishati yakupikia tu pia uchafu ambao unakuwa umetokana na mabaki haya unaweza kufanywa kama mbolea kwa mazao mbalimbali tunayoyalima hivyo ni vyema kila mwananchi kuhakikisha nyumbani kwake anamtambo huu

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad