Siasa Zanzibar :Amini Salimini Ajinadi kwa Wanachama wa CCM Jimbo la Mkwajuni Unguja Wakati wa Uzinduzi wa Kampeni. - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0676 643 633

Tuesday, 21 July 2015

Siasa Zanzibar :Amini Salimini Ajinadi kwa Wanachama wa CCM Jimbo la Mkwajuni Unguja Wakati wa Uzinduzi wa Kampeni.


Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo las Mkwajuni Zanzibar Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Ndg Khamis Mohammed Jecha akifungua rasmini Kampeni xza Wagombea Uwakilishi Ubunge na Udiwani wa Jimbo la Mkwajuni katika Tawi la CCM Moga A Wilaya ya Kaskazini Unguja jana 
Mgombea wa Ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Amini Salimini Amour Juma akiwahutubia Wananchi wa Tawi la CCM Moga A Kaskazini A Unguja wakati wa uzinduzi wa kampeni uliozinduliwa Rasmin Zanzibar katika Majimbo yote ya Uchaguzi kupitia Matawi yao na kujinadi wagombea kwa Wananchi ili kupata ridhaa za kuchaguliwa. 
 Mgombea Ubunge Jimbo la Mkwajuni akimwa Sera zake kwa Wananchi wa Tawi la CCM Moga A Wilaya ya Kaskazini A Unguja wakati wa kuaza kampeni kupita katika Matawi ya CCM kuomba ridhaa zao kuchaguliwa kukiwakilicha Chama katika uchaguzi Mkuu wa Ubunge mwishoni mwa mwaka huu.
 Amini Salimini akisisitiza jambo wakati akitowa sera zake kwa Wana CCM wa Moga Wilaya ya Kaskazini A Unguja jana katika viwanja vya tawi la CCM.
Viongozi wa CCM wanaosimamia kampeni za Wagombea wa Jimbo la Mkwajuni Zanzibar wakifuatilia kampeni hizo kwa wagombea wanaojieleza kwa Wananchi waliofika kuwasikiliza katika matawi ya CCM.
Wananchi wa Moga wakifuatilia Sera za Mgombea wa Ubunge wa Mkwajuni Amini Salimini Amour Juma, akimwaga sera zake kwa Wananchi wa Jimbo hilo.
Wanawake wa Tawi la CCM Moga wakimsikiliza Mgombea wa CCM Amini Salimini akizungumza na kutoa sera zake kwa Wananchi hao wakati wa uzinduzi wa kampeni zilizozinduliwa jana Zanzibar katika Matawi mbalimbali ya CCM katika Majimbo yao.
Makada wa CCM wakifuatilia kampeni za Wagombea wakati Mgombea Ubunge Amini Salimini akijieleza kwa wananchi hao katika tawi la CCM Moga. 

No comments:

Post a Comment