Mratibu
Mratibu
wa Bima ya Elimu kwa
Uwapendao kutoka Taasisi ya Kifedha ya Bayport
Financial Services, Ruth Bura, akizungumza na baadhi ya watumishi wa
shule ya sekondari James Sangu (hawapo pichani ) juu ya namna ya
kujiunga na fao hilo kabla ya kufanyika kwa zoezi la makabidhiano ya
hundi kwa Jaqline Ndyamkama ambaye ni mwanafunzi wa shule hiyo
yenye thamani ya Tsh 3,000,000, baada ya mama yake Anna Jelle kufariki
Dunia. Picha zote Emanuel Madafa, Mbeya.
|
Na Mwandishi
Wetu, Dar es Salaam
TAASISI
ya
Kifedha inayojihusisha na mambo ya mikopo ya Bayport Financial Services,
jana
imewakabidhi wanafunzi wawili hundi ya Sh Milioni tatu, itakayowawezesha
kila mwaka kupata Sh Milioni moja kwa kipindi cha miaka mitatu
mfululizo kwa ajili ya ada kwenye
shule zao wanazosoma kutokana na malipo ya Bima ya Elimu kwa uwapendao
inayoendeshwa na taasisi hiyo.
Wanafunzi
hao
ni Jacqueline Ndyamkana wa shule ya sekondari ya James Sangu na
Joceline
Ndyamkana wa shule ya awali, huku malipo hayo yakitokana na bima ya mama
yao aliyejulikana
kwa jina la Anna Jelle, ambapo kwa kupewa kiasi hicho cha fedha kila
mwaka, kutawafanya wasome bila usumbufu wowote katika kipindi hicho cha
miaka mitatu mfululizo.
Mratibu wa Bima ya Elimu kwa Uwapendao kutoka Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, Ruth Bura, akitoa ufafanuzi kuhusiana changamoto mbalimbali zinazowakibili wateja wao na namna ambavyo walivyo weza kuhudumia wateja wao. |
Alpha Akimu Meneja wa Kanda za Nyanda za juu Kusini akizungumza katika hafla hiyo.
Akizungumza
jana wilayani Mbozi, mkoani Mbeya, Mratibu wa Bima ya Elimu ya Bayport
Financial Sercices, Ruth Bura, alisema kwamba fedha hizo zinatoka kwa
ajili ya kuwezesha watoto hao wawili.
|
Baadhi ya walimu wa shule ya Sekondari James Sangu iliyopo Vwawa, Mbozi mkoani Mbeya, wakiuliza maswali kwa Mratibu wa
Bima ya Elimu kwa Uwapendao kutoka Taasisi ya Kifedha ya Bayport
Financial Services, Ruth Bura, (hayupo pichani) juu ya huduma zinazotolewa na Taasisis hiyo.
|
Shughuli ikiendelea
Watu wakiuliza maswali
Makabidhiano yakiendelea
Makabidhiano ya hundi yakiendelea
Makabidhiano yakiendelea
Picha ya pamoja
Asante kwa hundi
Alisema
taasisi yao iliamua kuanzisha huduma hiyo ya bima ya elimu kwa
uwapendao ili kuhakikisha kwamba watoto wanaendelea kupata elimu zao,
hata inapotokea wazazi wao wanafariki Dunia. “Ndugu
yetu Anna Jelle alijiunga na huduma yao Aprili 14 mwaka jana, ambapo
mwaka huu ilitokea bahati mbaya akafariki Dunia, hivyo tukaona tuwape
watoto hawa stahiki zao ili waendelee na masomo yao.
“Watoto
hawa watapata Sh Milioni moja kwa kila mwaka na watapewa fedha hizi kwa
kipindi cha miaka mitatu mfululizo, tukiamini kuwa tunaweza kurahisha
masomo yao japo kwa kipindi hiki ambacho mzazi wao hayupo,” alisema. Naye
Jacqualine aliishukuru Bayport kwa kuanzisha huduma hiyo muhimu,
akiamini kwamba kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo anaweza kuwa
katika mazingira mazuri kwenye masomo yake na mdogo wake.
Kwa
mujibu wa Ruth, malipo ya kila mwezi kwa fao la Bronze ni Sh 3500 tu,
huku mafao yake yakiwa ni Sh 1,800,000 na makato ya bima ya Silver ni Sh
7,000 na fao lake ni Sh 3,700,000 na Gold akilipwa mteja Sh 7,500,000
wakati makato yake yakiwa ni Sh 12,000 tu kwa mwezi na kusisitiza kwamba
ambapo mbali na
bima, taasisi yao pia inatoa huduma ya mikopo ya bidhaa bila kusahau
mradi wa viwanja vya Vikuruti, wilayani Kibaha mkoani Pwani.
No comments:
Post a Comment