Matukio : Mahakama Yamsomea Maelezo ya Awali Tido Mhando Anayekabiliwa na Mashtaka Matano - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


24 Feb 2018

Matukio : Mahakama Yamsomea Maelezo ya Awali Tido Mhando Anayekabiliwa na Mashtaka Matano


Na Karama Kenyunko, blogu ya Jamii.


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema, Aprili 28 mwaka huu, itamsomea maelezo ya awali aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Shirika la Utangazaji uTanzania (TBC), Tido Mhando (Pichani), anayekabiliwa na mashtaka matano. Hatua hiyo imekuja baada ya Wakili wa Tido, Ramadhani Maleta kuiomba Mahakama iwapatie muda wa kupitia maelezo ya awali ili aweze kushauriana na mteja wake kabla ya kusomwa.


Kesi hiyo leo ilikuja kwa ajili ya mshtakiwa Mhando kusomewa maelezo ya awali ambapo mwendesha mashtaka wa Takukuru, Leonard Swai alidai wako tayari kumsomea. Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo na wakili Maleta aliomba apewe muda kwa sababu alipatiwa maelezo hayo ya awali na upande wa mashtaka wakati wakiwa mahakamani hapo.


Swai alipinga hoja hiyo na kudai kwa utaratibu wanapaswa kumsomea mshtakiwa maelezo hayo ya awali na Mahakama imuulize kipi anakubali na kipi anachokikataa na kwamba wanaweza kupitia kwa dakika tano.


Hata hivyo Hakimu Mfawidhi, Victoria Nongwa aliwapatia muda hadi Februari 28,mwaka 2018 ambapo Tido atasomewa maelezo ya awali. Tido anakabiliwa tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia Serikali hasara ya Sh milioni 887.1 Inadaiwa Juni 16, mwaka 2008 akiwa Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Tido ambaye alikuwa mkurugenzi wa TBC, kwa makusudi alitumia madaraka yake vibaya kwa kusaini mkataba wa kuendesha na utangazaji wa vipindi vya televisheni kati ya TBC na Channel 2 Group Corporation (BV1) bila ya kupitisha zabuni, kitu ambacho ni kinyume na Sheria ya Manunuzi na kuinufaisha BVl. Katika shtaka la pili, Tido anadaiwa kutumia vibaya madaraka yake Juni 20,mwaka 2008 aliposaini makubaliano kwa utangazaji wa digitali duniani kati ya TBC na BVl.


Katika shtaka la tatu, Swai alidai Agosti 11,mwaka 2008 na Septemba mwaka 2008 akiwa Dubai, Tido alitumia vibaya madaraka yake kusaini mkataba wa makubaliano kwa ununuzi, usambazaji kufunga vifaa vya usambazaji na mnara wa utangazaji kati ya TBC na BVI na kuifaidisha BVI.


Katika shtaka la nne, Wakili Swai alidai Novemba 16,mwaka 2008 akiwa Dubai, Tido alitumia vibaya madaraka yake kusaini mkataba wa makubaliano kwa kuendesha miundombinu ya utangazaji (DTT Broadcast Infrastructure) kati ya TBC na BVI na kuinufaisha BVI. Katika shtaka la mwisho, Swai alidai kati ya Juni 16 na Novemba 16, mwaka 2008 akiwa UAE, Tido aliisababishia TBCli hasara ya Sh887,122,219.19.

Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Tido Mhando (Pichani), anayekabiliwa na mashtaka matano akiwa katika chumba cha mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akisubiri kusomewa kesi yake.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad