NAPE: Hata kwa goli la mkono lazima tuibuke washindi Gabon - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


25 Feb 2017

NAPE: Hata kwa goli la mkono lazima tuibuke washindi Gabon


WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amesema hata kwa goili la mkono ni lazima Serengeti Boys warejee nyumbani wakiwa ama na kombe au wakiwa wamefuzu kushiriki kombe la dunia kwa kuwa moja ya timu mbili zinazohitajika. Kauli ya Waziri Nape ameitoa leo asubuhi wakati akifungua mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017 safari kuelekea Anfield ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 100 tangu benki hiyo kuanzishwa mwaka 1917 yaliyoanza kutimua vumbi katika viwanja vya JK Park Kidongo Chekundu, Gerezani. Alisema haiwezekani taifa hili kuwa na Waziri mjanja kama Nape halafu Serengeti Boys inakosa kombe huko Gabon na nafasi ya ushiriki Kombe la dunia. Pamoja na kauli yake hiyo Waziri Nape aliiomba Benki ya Standard Chartered kushiriki katika jukumu la kuhakikisha kwamba Serengeti Boys ama inarejea na kombe au inafuzu miongoni mwa timu mbili zitakashiriki Kombe la Dunia.

Picha juu na chini ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (katikati), Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Tanzania Sanjay Rughani (mwenye kofia) na Mwenyekiti wa Kamati ya uamuzi TFF, Salum Chama (wa tatu kulia) wakijumuika kwa pamoja na washiriki wa mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017 (Road to Anfield) kutoka makampuni mbalimbali kupasha misuli moto yaliyoanza kutimua vumbi leo kwenye viwanja vya JK Park Kidongo Chekundu, Gerezani jijini Dar es Salaam.(Picha na thebeautytz.co.tz)

Alisema kwa sasa serikali inawaomba wadau kushiriki katika kuhakikisha kwamba Kambi ya Serengeti Boys inaimarika na kuwezesha kuwa na kikosi cha ushindi. Aliishukuru Benki hiyo kwa kuhakikisha kwamba inainua michezo nchini kwa kusaidia kunyanyua na timu ya wanawake na kusema kitendo cha wao kuileta Dunia nchini Tanzania (Liverpool na mashabiki wake na michuano ya kuelekea Anfield) ni cha kushukuriwa sana. Aliishukuru pia kwa kumleta nguli John Barnes na kulitaka Shirikisho la kabumbu nchini (TFF) kuhakikisha kwamba wanatumia nafasi hiyo kuwaweka sawa pia kisaikolojia vijana wa Serengeti Boys. Alisema ujio wa Barnes unaneema kubwa hasa ratiba yake ya kukutana na vijana wa Serengeti. Pamoja na kuzungumzia Serengeti Boys, Waziri Nape aliitaka jamii kuthamini michezo na kushiriki kwa kuwa huleta afya na kujenga umoja. Alitaka timu zote 32 zinazowania kufuzu kucheza ngwe ya Afrika mashariki kucheza kwa bidii na furaha na kuhakikisha wanapata ushindi halali ili waweze kuiwakilisha vyema Tanzania katika michuano ya Afrika Mashariki jumamosi ijayo. Washindi wa mwaka jana timu ya Mwananchi ilitolewa mapema katika mashindano hayo ambayo yanaendelea hadi jioni ya leo wakati mshindi atakapopatikana. Mshindi wa mashindano hayo atapambana na washindi kutoka Kenya na Uganda ambao nao leo wanawasaka washindi wao katika nchi hizo.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (katikati), Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Tanzania Sanjay Rughani (mwenye kofia) na Mwenyekiti wa Kamati ya uamuzi TFF, Salum Chama (kushoto kwa Waziri Nape) katika picha ya pamoja baada ya kukabidhi bendera kwa washiriki kutoka makampuni mbalimbali wa mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017 (Road to Anfield) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 100 tangu benki hiyo kuanzishwa mwaka 1917 yaliyoanza kutimua vumbi leo kwenye viwanja vya JK Park Kidongo Chekundu, Gerezani jijini Dar es Salaam.

Zawadi ya timu itakayoshinda Afrika Mashariki ni safari ya kwenda Liverpool na kuangalia mechi zitakazpigwa na timu hiyo katika uwanja wa Anfield mwezi Mei. Aidha timu hiyo itapata nafasi ya kutembelea uwanja wa Anfield na kukutana na magwiji mbalimbali wa Liverpool. Safari hiyo ya timu ya watu saba italipiwa na Benki ya Standard Chartered ambayo inafadhili timu ya Liverpool yenye mashabiki zaidi ya milioni 700 duniani.

Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Tanzania Sanjay Rughani akisoma risala kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (hayupo pichani) wakati wa mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017 (Road to Anfield) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 100 tangu benki hiyo kuanzishwa mwaka 1917 yaliyoanza kutimua vumbi leo kwenye viwanja vya JK Park Kidongo Chekundu, Gerezani jijini Dar es Salaam.

Awali Mwenyekiti wa waamuzi Salum Umange Chama ambaye alimwakilisha Rais wa TFF Jamal Malinzi aliishukuru benki ya Standard kwa kuwa championi wa michezo na kwa kufadhili mafunzo ya wamuuzi na timu ya wanawake. Aliitaka Benki hiyo kuendelea kufadhili michezo nchini ili iweze kukua. Wakati huo huo Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Tanzania Sanjay Rughani Sanjay amesema kwamba benki yake inaona fahari kuwa mgeni wa michuano hiyo kuelekea Anfield kwa nchi za Afrika Mashariki na kuwataka washiriki wakaze nia ya kutwaa ubingwa. Alisema mashindano ya mwaka huu yanaendana na miaka 100 ya shughuli za benki hiyo nchini Tanzania.

Mwenyekiti wa Kamati ya uamuzi TFF, Salum Chama akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kubariki mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017 (Road to Anfield) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 100 tangu benki hiyo kuanzishwa mwaka 1917 yaliyoanza kutimua vumbi leo kwenye viwanja vya JK Park Kidongo Chekundu, Gerezani jijini Dar es Salaam.

Pia alisema anaona fahari kuwapeleka washindi kuzuru uwanja wa kihistoria wa Anfield na kuwatembelea Liverpool FC timu iliyoanzishwa 1892 nchini Uingereza hadi kwa wananchi wa kawaida kwa kuanzisha mashindano hayo ambapo timu inacheza kwa dakika 10 ikiwa na wachezaji watano na wawili wa akiba. Mashindano hayo yapo katika bara zote ambapo benki ya Standard Chartered inafanyakazi.

Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akizungumza na washiriki wa mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017 (Road to Anfield) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 100 tangu benki hiyo kuanzishwa mwaka 1917 yaliyoanza kutimua vumbi leo kwenye viwanja vya JK Park Kidongo Chekundu, Gerezani jijini Dar es Salaam.





Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (katikati) akibadilishana mawazo na Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Tanzania Sanjay Rughani wakati mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017 (Road to Anfield) yakiendelea katika viwanja vya JK Park Kidongo Chekundu, Gerezani jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya uamuzi TFF, Salum Chama.



Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akizundua rasmi mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017 safari kuelekea Anfield kwa kupiga mpira kwenye viwanja vya JK Park Kidongo Chekundu, Gerezani jijini Dar es Salaam.


Mchezaji wa Benki ya Standard Chartered (jezi nyeupe) akichuana vikali na wenyeji wa JK Park (jezi za kijani) kwenye mechi ya kwanza ya dakika kumi wakati wa mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017 ya safari kuelekea Anfield ambapo timu ya JK Park iliibuka kidedea kwa bao 1-0.





Mchezaji wa Mwananchi Communication (tisheti nyeupe) akijaribu kumtoka mchezaji wa ORYX kwenye wa mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017 safari kuelekea Anfield ambapo timu ya ORYX Park iliibuka kidedea kwa bao 2-0.



Mshehereshaji wa mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017 (Road to Anfield), Maulid Baraka wa Kitenge (kulia) akibadilishana mawazo na Meneja Miradi wa Executive Solutions, Hilda Ngowi (katikati) na Mhasibu wa Executive Solutions, Mapunda (kushoto) wakati wa mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017 (Road to Anfield) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 100 tangu benki hiyo kuanzishwa mwaka 1917 yaliyoanza kutimua vumbi leo kwenye viwanja vya JK Park Kidongo Chekundu, Gerezani jijini Dar es Salaam.


Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Tanzania Sanjay Rughani (kushoto) akibadilishana mawazo na Mkuu wa kitengo cha makampuni makubwa wa benki hiyo, Jaffer Machano wakati wa mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017 (Road to Anfield) ) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 100 tangu benki hiyo kuanzishwa mwaka 1917 yaliyoanza kutimua vumbi leo kwenye viwanja vya JK Park Kidongo Chekundu, Gerezani jijini Dar es Salaam.



Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (katikati) kwenye picha ya pamoja na Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Tanzania Sanjay Rughani (wa pili kushoto), Mkuu wa kitengo cha makampuni makubwa wa benki hiyo, Jaffer Machano (wa pili kulia), Mwenyekiti wa Kamati ya uamuzi TFF, Salum Chama (kulia) na Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba (kushoto) wakati mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017 (Road to Anfield) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 100 tangu benki hiyo kuanzishwa mwaka 1917 yaliyoanza kutimua vumbi leo kwenye viwanja vya JK Park Kidongo Chekundu, Gerezani jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad