Afya : Tutaendelea kutatua Changamoto Zinazowakabili Wahudumu Muhimbili - Prof. Museru - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


20 Jan 2017

Afya : Tutaendelea kutatua Changamoto Zinazowakabili Wahudumu Muhimbili - Prof. Museru


Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili ( MNH), Profesa Lawrence Museru  amekutana na wahudumu wa Afya katika hospitali hiyo pamoja na mambo mengine amewasisitiza kufanya kazi kwa bidii na kwamba uongozi wa hospitali hiyo utaendelea kutatua changamoto zinazowakabili.
Pia, mkurugenzi huyo amewataka wahudumu hao kuzingatia maadili ya kazi ili kutoa huduma bora kwa wagonjwa.


Profesa Museru ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es salaam katika mkutano na baadhi ya wahudumu wa afya uliolenga kumpongeza kwa kuteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo.


Profesa Museru amesema licha ya wahudumu hao kukabiliwa changamoto mbalimbali , lakini hawanabudi kufanya kazi kwa bidii kwani jukumu lao ni kutoa huduma bora.


" Nawapongeza kwa kazi nzuri mnayofanya hatua ambayo imesaidia kupunguza malalamiko wakati wa kutoa huduma , ingawa bado kuna changamoto lakini hatua budi kutoa huduma bora na sisi tutaendelea kutatua changamoto hizo kadiri inavyowezekana ili kuhakikisha mazingira yetu ya kazi yanakua bora," amesema Profesa Museru.


Katika mkutano huo wahudumu hao wamewasilisha ajenda 14 ikiwamo ombi la kupatiwa mafunzo ili kuongeza ufanisi na kuboresha utendaji kazi wao.

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akifafanua jambo kwenye mkutano huo. Kulia ni Mkurugenzi wa Uuguzi, Agnes Mtawa wa hospitali hiyo.

Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk Mtemi Sufiani Baruani, Mkurugenzi wa Uuguzi, Agnes Mtawa, Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Profesa Lawrence Museru, Kaimu Mkuu wa Idara ya Utawala, Leila Komba, Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Shirikishi, Dk. Praxeda Ogweo na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba, Hedwiga Swai wakiwasikiliza wahudumu wa hospitali hiyo katika mkutano uliowahusisha viongozi hao. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa jengo la maabara kuu.

Mkurugenzi wa Uuguzi, Agnes Mtawa akisisitiza jambo kwenye mkutano huo.

Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Shirikishi, Dk. Praxeda Ogweo wa hospitali hiyo akizungumza na wahudumu katika mkutano.

Mmoja wa wafanyakazi wa hospitali hiyo, Joseph Oloch akizungumza kwenye mkutano huo.



Baadhi ya wahudumu hao wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru.

Wahudumu wakifuatilia jambo kwenye mkutano huo.

Mwenyekiti wa TUGHE, Tawi la Muhimbili, Mziwanda Salumu Chimwege akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru zawadi kutoka kwa wahudumu wa hospitali hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad