Kilimo Kwanza : Taasisi ya African Relief yaanzisha kilimo cha Umwagiliaji Chumbi, Rufiji. - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


8 Dec 2016

Kilimo Kwanza : Taasisi ya African Relief yaanzisha kilimo cha Umwagiliaji Chumbi, Rufiji.



Mkurugenzi wa Taasisi ya African Relief Organization, Samy Mohammed Elazeb (kulia) akisimamia trekta likilima shamba lenye ukubwa wa ekali 2500 eneo la Khanga, katika Kijiji cha Chumbi C, wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani mwishoni mwa wiki.Taasisi hiyo itaanza uzalishaji wa mazao ya mahindi na mpunga.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

Mwenyekiti wa Taasisi ya African Relief Organization, Abdallah Ndauka akisimamia trekta likilima shamba lenye ukubwa wa ekali 2500 eneo la Khanga, katika Kijiji cha Chumbi C, wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani mwishoni mwa wiki.Taasisi hiyo itaanza uzalishaji wa mazao ya mahindi na mpunga.

Ndauka akizungumza na vyombo vya habari kuhusu mradi huo

Vibarua akifyaka vichaka kusafisha shamba hilo

Mwenyekiti wa Taasisi ya African Relief Organization, Abdallah Ndauka na Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Samy Mohammed Elazeb (kulia) wakisimamia trekta likilima shamba lenye ukubwa wa ekali 2500 eneo la Khanga, katika Kijiji cha Chumbi C, wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani mwishoni mwa wiki.Taasisi hiyo itaanza uzalishaji wa mazao ya mahindi na mpunga.

Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Samy Mohammed Elazeb akisimamia maandalizi ya shamba hilo

Ndauka na Samy Mohammed Elazeb wakijadiliana jambo

Mratibu wa Mradi huo, Peter Ambilikile (kushoto) akifafanua jambo

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kijiji cha Chumbi C, Utete, wilayani Rufiji,mkoani Pwani, Salim Mtimbuko akielezea mbele ya wanahabari kijijini hapo mwishoni mwa wiki, jinsi Kijiji hicho, kilivyonufaika na misaada mbalimbali iliyotolewa kwao na Taasisi ya African Relief Organization. Kijiji hicho kimepatiwa misaada ya kisima cha maji, ukumbi wa mikutano, majengo ya ofisi na ukarabati wa shule ya Chumbi.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kijiji cha Chumbi C, Utete, wilayani Rufiji,mkoani Pwani, akielezea mbele ya wanahabari kijijini hapo mwishoni mwa wiki, jinsi Kijiji hicho, kilivyonufaika na misaada mbalimbali iliyotolewa kwao na Taasisi ya African Relief Organization. Kijiji hicho kimepatiwa misaada ya kisima cha maji, ukumbi wa mikutano, majengo ya ofisi na ukarabati wa shule ya Chumbi.

Samy Mohammed Elazeb (kushoto), na mwanakijiji wakiziba maji kwenye mabomba ya kisima kilitolewa msaada na taasisi hiyo kwa Kijiji cha Chumbi C



Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Chumbi C, akikinga maji kwa mkono katika kisima hicho.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kijiji cha Chumbi C, Utete, wilayani Rufiji,mkoani Pwani, Salim Mtimbuko, akionesha ukumbi wa Kijiji ambao umejengwa kwa msaada wa Taasisi hiyo.


Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kijiji cha Chumbi C, Utete, wilayani Rufiji,mkoani Pwani, Salim Mtimbuko akionesha jengo la ofisi za kijiji hicho, lililojengwa kwa msaada wa taasisi hiyo.


Nyumba anayoishi Ofisa Kilimo wa Kijiji hicho

Post Top Ad