Matukio : Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Akutana na wawekezaji kutoka Korea ya Kusini - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


28 Sept 2016

Matukio : Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Akutana na wawekezaji kutoka Korea ya Kusini


 Waziri Mkuu , Kassim Majaliwa akikabidhiwa jezi yanye maneno  Hapa Kazi Tu  iliyotolewa na wawekezaji kutoka Korea ya Kusini waliokuja nchini kuona fursa mbalimbali za uwekezaji.  Awali Waziri Mkuu alizungumza na wawekezaji hao ofisini kwake jijini Dar es salaam Septemba 27, 2016. Kulia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, ambaye pia ni Mbunge wa Ilemela, Angelina Mabula.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa makampuni mbalimbali kutoka Korea ya Kusini ambao wamekuja Tanzania kuona fursa mbalimbali za uwekezaji. Mazungumzo hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam  Septemba 27, 2016. Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni Mbunge wa Ilemela, Angelina Mabula
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika  picha ya pamoja na  viongozi wa makampuni mbalimbali ya Korea Kusini ambao wapo nchini kuona fursa  mbalimbali za uwekezaji  nchini. Picha hiyo ilitanguliwa na mazungumzo yaliyofanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Septemba 27. Watatu kulia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,  Angelina Mbula.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad