Matukio : TANROADS na TBA zaagizwa kufanya Tathmini kwenye miundombinu ya Barabara na majengo ya Serikali - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


26 Sept 2016

Matukio : TANROADS na TBA zaagizwa kufanya Tathmini kwenye miundombinu ya Barabara na majengo ya Serikali


Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga  ameuagiza  uongozi wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), na Wakala wa Majengo Nchini (TBA), mkoa wa Kagera kufanya tathmini ya kina kwenye miundombinu ya barabara, madaraja na majengo ya Serikali yalioathirika na tetemeko la ardhi.

Eng. Nyamhanga ametoa agizo hilo Mkoani Kagera mara baada ya kukagua athari za tetemeko la ardhi katika barabara za Bukoba- Mtukula, Kyaka-Bugene na jengo la Kituo cha Pamoja cha Forodha cha Tanzania na Uganda  ambapo amesema ni muhimu kufanya utafiti wa kitaalam katika miundombinu hiyo kabla ya hatua za ukarabati kuanza.

Amesema kufanyika kwa utafiti huo utasaidia kubaini athari nyingine zilizojificha ambazo zimetokana na tetemeko hilo.
“Undeni kikosi kazi cha wataalam maramoja waweze kuchunguza ili kujua sehemu mbalimbali zilizoathirika ili tuweze kuzitengeneza mapema iwezekanvyo”, amesema Eng. Nyamhanga.

Katika hatua nyingine Eng. Nyamhanga amemuagiza Mkandarasi wa Kampuni ya M/S China Henan International Cooperation Group Co. Ltd (CHICO) inayojenga barabara ya Kyaka-Bugeni (KM 59.1) kumaliza kipande cha Kilomita mbili katika barabara hiyo ifikapo mwezi Disemba mwaka huu.

Amesema kuwa kukamilika kwa kipande hicho kutaimarisha hali ya usafiri wa wananchi katika wilaya za Bukoba na Karagwe na hivyo kuhuisha shughuli za kiuchumi kwa wakazi wa Mkoa wa Kagera.
Eng. Nyamhanga yupo mkoani Kagera kukagua athari za uharibifu wa miundombinu kufuatia tetemeko la ardhi lililopiga mikoa ya Kagera, Mara na Mwanza Septemba 10 mwaka huu na kusababisha vifo vya watu takribani 17, majeruhi zaidi ya 100, uharibifu wa nyumba takribani 800 na miundombinu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga (kushoto) akikagua sehemu ya barabara ya Bukoba-Mtukula ambayo imepata athari kutokana na tetemeko la ardhi lilitokea Mkoani Kagera hivi karibuni. Kushoto ni Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Mkoa wa Kagera Eng. Andrea Kasamwa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga (kushoto), akitoa maelekezo kwa Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Mkoa wa Kagera Eng. Andrea Kasamwa (kulia) wakati alipokagua Daraja la Kyaka katika Mto Kagera.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga (wa pili kulia) akitoa maelekezo kwa Mkandarasi wa kampuni ya M/S China Henan International Cooperation Group Co. Ltd (CHICO) inayojenga barabara ya Kyaka-Bugeni (KM59.1), Mkoani Kagera.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga (kulia), akikagua daraja la Mwise lililopo katika barabara ya Bukoba- Mtukula.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga (wa tatu kushoto), akikagua kipande cha Barabara ya Kyaka-Bugeni (KM59.1 ) inayojengwa kwa kiwango cha lami, Mkoani Kagera.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga (wa pili kulia), akitoa maelekezo kwa Afisa Mfawidhi wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Bw. Samweli Mori wakati alipokagua jengo la Kituo cha Pamoja cha Forodha ambacho kimeathirika na tetemeko la ardhi lililopo Mtukula Mkoani Kagera.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga (wa pili kulia), akikagua jengo la Kituo cha Pamoja cha Forodha ambacho kimeathirika na tetemeko la ardhi lililopo Mtukula Mkoani Kagera. Picha na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad