Utafiti : Vyombo vya Habari Asilia hususan Magazeti viko mbioni kupotea kabisa , wakati vya Digitali vyaendelea Kupeta - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


4 May 2016

Utafiti : Vyombo vya Habari Asilia hususan Magazeti viko mbioni kupotea kabisa , wakati vya Digitali vyaendelea Kupeta


Vyombo vya habari vya asilia hususan magazeti vinakufa. Hivi sasa vyombo hivyo vinajikongoja kutokana na  mauzo hafifu  na mdororo wa mapato kutoka matangazo na kupunguza wafanyakazi. 
Ila wakati idadi ya wasomaji wa habari mtandaoni ikizidi kukua, wanaoperuzi mtandaoni  humo hawatumii muda mwingi kwenye magazeti tando, utafiti wa Pew Research Centre unaeleza. 

Katika utafiti wake wa hali ya vyombo vya habari 2015 ("State of the News Media 2015,”) imeonesha kwamba katika vyombo vya habari vya karatasi (print media), Digitali na TV, imeonesha Dhahiri kwamba magazeti yanaelekea kuzimu. 
Utafiti huo umetolea mfano magazeti makubwa ambapo wasomaji wake wa mtandaoni wamewashinda kwa mbali kwa idadi ya wasomaji wa makaratasini, ambapo gazeti kubwa sana la New York Times la Marekani limetangaza kuwa nakala zake zipatazo 650,000 kwa wiki zimepitwa kwa mbali sana na wa mitandaoni 
 Hivi sasa kuna mjadala mitandaoni endapo kama Tanzania iko ama itafika huko. Mabishano ni makali ambapo wa makaratasini wanashikilia msimamo wao kuwa nchini hapa tasni ya habari mtandaoni bado ni change sana kuweza kutishia amani ya magazeti. 
Upande wa digitali unajibu kwamba endapo kama kuna wahariri viburi wanaobeza kasi ya mitandao, basi wakae mkao wa kulala njaa muda si mrefu ujao, maana ni wachache wanaoendelea kupata habari kwa njia asili ya magazeti. 
Upande wa digitali umeyasifia magazeti ya Global Publishers na la Mwananchi  anbayo ni dhahiri yana wahariri wanaokwenda na wakati na wanaojua nini wanachokifanya kwa kuanza na mapema kuogelea bahari ya maendeleo ya tasnia kwa vitendo kwa kuwa na vitengo vya mtandao vinavyopelekesha mbio magazeti yanayobeza technolojia hio kwa kubuni.
"Ni kweli kwamba Tanzania ni bado sana kiteknolojia na miundombinu kiasi cha habari za mtandaoni zikatishia uhai wa habari za makaratasini, lakini si uwongo kwamba ukizingatia uharaka na gharama pamoja na kwenda na wakati muda si mrefu print media itakwenda na maji", amesema blogger mmoja ambaye pia ni mwanahabari kwenye moja ya magazeti makubwa nchini.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad