Usafi wa Mazingira : Mkoa wa Dodoma Umeanza Kutekeleza Agizo la Mhe. Rais Magufuli la Kufanya Usafi siku ya Uhuru 9 Desemba ,2015 - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


29 Nov 2015

Usafi wa Mazingira : Mkoa wa Dodoma Umeanza Kutekeleza Agizo la Mhe. Rais Magufuli la Kufanya Usafi siku ya Uhuru 9 Desemba ,2015

 Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Ndg. Rehema Madenge (mbele walioingia mtaroni) na watumishi wengine wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wakishiriki zoezi la kusafisha mitaro ya maji ya mvua eneo la Bahi Roadmapema leo ikiwa ni mwanzo wa utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais la kutumia siku ya uhuru 9 Disemba kufanya usafi wa mazingira.
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Ndg. Rehema Madenge (katikati aliyeshika koleo) akiongea kuhamasisha zoezi la watumishi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa kusafisha mitaro ya maji ya mvua eneo la Bahi Road mapema leo
 Wafanyakazi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na Tume ya Maendeleo ya Ushirika wakijiorodhesha baada ya kumaliza zoezi la usafi wa mazingira mapema leo ikiwa ni mwanzo wa utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais la kutumia siku ya uhuru 9 Disemba kufanya usafi wa mazingira, orodha hiyo itatumika kuwabaini watumishi ambao hawajashiriki zoezi la usafi.
 Wafanyakazi wa Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Tume ya Maendeleo ya Ushirika na Manispaa ya Dodoma wakishiriki zoezi la kusafisha mitaro ya maji ya mvua eneo la Bahi Road mapema leo ikiwa ni mwanzo wa utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais la kutumia siku ya uhuru 9 Disemba kufanya usafi wa mazingira.
 Wafanyakazi wa Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Tume ya Maendeleo ya Ushirika na Manispaa ya Dodoma wakishiriki zoezi la kusafisha mitaro ya maji ya mvua eneo la Bahi Road mapema leo ikiwa ni mwanzo wa utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais la kutumia siku ya uhuru 9 Disemba kufanya usafi wa mazingira.
 Mhandisi wa Maji wa Mkoa wa Dodoma Bazil Mwiserya akishiriki zoezi la kusafisha mitaro ya maji ya mvua eneo la Bahi Road mapema leo ikiwa ni mwanzo wa utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais la kutumia siku ya uhuru 9 Disemba kufanya usafi wa mazingira.
 Watumishi wa Manispaa ya Dodoma wakishiriki zoezi la kufanya usafi kwa kufyeka magugu eneo la makaburi ya Bahi Road mapema leo ikiwa ni mwanzo wa utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais la kutumia siku ya uhuru 9 Disemba kufanya usafi wa mazingira.
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Ndg. Rehema Madenge (katikati aliyeshika koleo) akiongoza zoezi la watumishi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa kusafisha mitaro ya maji ya mvua eneo la Bahi Road mapema leo
Wafanyakazi wa Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Tume ya Maendeleo ya Ushirika na Manispaa ya Dodoma wakishiriki zoezi la kusafisha mitaro ya maji ya mvua eneo la Bahi Road mapema leo ikiwa ni mwanzo wa utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais la kutumia siku ya uhuru 9 Disemba kufanya usafi wa mazingira.
Na Mwandishi wetu,
Mkoa wa Dodoma umeanza rasmi kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli lililotaka kufanyika kwa usafi wa mazingira katika maeneo mbalimbali ya nchi siku ya tarehe 9 Disemba, 2015 kama mojawapo ya maadhimisho ya siku ya uhuru na kuwataka viongozi na wataalamu kusimamia utekelezaji wa agizo hilo.
Uongozi wa Mkoa umeamua kuanza mapema zoezi la ufanyaji usafi pasipo kusubiri tarehe 9 Disemba na umepanga kuwa zoezi hilo litakuwa endelevu likihusisha usafi wa kila siku na usafi wa siku zote za Jumamosi kuanzia saa 1:00 hadi saa 3:00 asubuhi.
Taasisi mbalimbali zilizopo Mkoani Dodoma zimetumia Jumamosi ya leo Novemba 28, 2015 kushirikiana na wananchi kufanya usafi kwenye maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Dodoma ambapo Viongozi na Watumishi wote wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Ofisi ya Tume ya Maendeleo ya Ushirika na Manispaa ya Dodoma wamefanya usafi eneo la Bahi Road kuelekea Nkuhungu kwa kuondoa taka na michanga kwenye mitaro ya maji ya mvua, kufyeka na kuchoma taka eneo la makaburi ya Kizota.
Kwa mujibu wa Ratiba ya usafi iliyotolewa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma, Mamlaka ya majisafi na usafi wa Mazingira mjini Dodoma-DUWASA ilifanya usafi eneo la kuanzia ofisi za waziri mkuu (Mtaa wa Mahakamani) hadi  ofisi za hazina ndogo.
TANESCO Mkoa wa Dodoma walisafisha eneo la kituo cha kuuzia mafuta cha BP Capital hadi soko la Sabasaba. Taasisi nyingine ni pamoja na jeshi la Magereza ambapo lilifanya usafi kuanzia mzunguko wa barabara ya kuelekea Bahi hadi maeneo ya magorofa mengi wakati mabenki yalisafisha mitaa na barabara zinazopita mbele ya majengo yao ya benki na Wakala wa Barabara TANROADS wao walisafisha kuanzia kituo cha mabasi ya mikoani hadi soko la Sarafina.
Kwa upande wa wananchi walioshiriki zoezi hilo la kufanya usafi, wamepongeza utaratibu na kusema utasaidia kuweka mji katika mazingira safi. Akiwawakilisha wananchi walioshiriki zoezi hilo, Mkazi wa Dodoma Onesmo Stephano alielezea kuwa utaratibu huo wa viongozi wa Mkoa na watumishi wa serikali kushiriki kufanya usafi unawatia hamasa kubwa wananchi nao kushiriki pale wanapoona viongozi wao wanashiriki kufanya nao usafi.
Mapema mwanzo wa wiki Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa alibainisha kuwa siku ya tarehe 9 Disemba itakuwa siku ya kutathimini kazi ya usafi inayoendelea kufanyika ndani ya Mkoa, pia utafanyika usafi kwenye maeneo ya huduma za jamii kama masoko na Hospitalini.
Maagizo yaliyotolewa wakati wa kupanga mikakati ya utekelezaji wa agizo la kufanya usafi kwenye Mkoa wa Dodoma ni pamoja na mamlaka za serikali za mitaa katika ukaguzi na usimamizi wa zoezi la usafi kwenye  maeneo ya makazi na shughuli mbalimbali wafanye  ukaguzi wa vyoo.
Vilevile ukaguzi kwa kazi iliyofanyika ya usafi wa mazingira ya makazi, maeneo ya huduma za jamii, maeneo ya utupaji taka. Maelekezo mengine ni pamoja na matumizi ya sheria ndogo kama kutoa ILANI, Makatazo na adhabu za Faini kwa makosa ya uchafuzi wa mazingira.

Uongozi wa Mkoa wa Dodoma umeelezea kuwa zoezi hili la kufanya usafi wa mazingira kila siku na usafi wa pamoja wa kila siku za jumamosi utasaidia kupunguza magonjwa mengi yatokanayo na uchafu wa mazingira kama vile kipindupindu, kuhara na magonjwa mengine ya milipuko na kwa sasa wanasubiri Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma kutoa ratiba ya zoezi la usafi la Jumamosi ijayo ya Disemba 5, 2015.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad