Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa Abdalla Bulembo wa kwanza kushoto Mbunge wa Kikwajuni Mhe Hamad Masauni na Kada wa CCM Abass Bahari wakijiandaa kuelekea kukagua timu hizo wakati wa Bonaza hilo linaloendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja usiku kwa michezo miwi kila siku.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa Mhe Abdalla Bulembo akisalimiana na wachezaji wa timu ya Muembeladu kabla ya kuaza kwa mchezo huo wa Bonaza katika viwanja vya mnazi mmoja Zanzibar, Bonaza hilo limedhaminiwa na Mbunge wa Kikwajuni kuinua vipaji vya Vijana katika mchezo wa Soka Zanzibar.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa Mhe Abdalla Bulembo akizungumza na wanamichezo wakati wa mchezo wa Bonaza Kombe la Masauni na kuwataja vijana kukuza michezo ndio mafanikia yao kujipatia ajira, Michezo huleta amani na utulivu katika nchi. Na kuahidi timu itakayoshinda katika mchezo huo ataizawadia shilingi laki moja. kwa bahati mbaya timu hizo zimetoka sare na kukabidhiwa kila moja shilingi 50,000/- baada ya kumalizika kwa mchezo huo wa sare ya 2--2
Mchezaji wa timu ya Muembeladu akimiliki mpira huku mchezaji wa Rahaleo akijiandaa kumzuiya wakati wa mchezo wa Bonaza Masauni Cup.
Wachezaji wa Rahaleo na Muembeladu wakiwania mpira katika mchezo wa Bonaza Masauni Cup linalofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja usiku.
Wapenzi wa mchezo wa soka Zanzibar wakifuatilia michezo ya Bonaza ya Kombe la Mbunge wa Kikwajuni Mhe Hamad Masauni. Masauni Cup.Bonaza
Kocha wa timu ya Muembeladu akitowa maelekkezo kwa wachezaji wake wakati wa mchezo wao na timu ya Rahaleo uliofanyika viwanja vya mnazi mmoja Zanzibar timu hizo zimetoka sare ya 2--2
Mchezaji wa timu ya Muembeladu akimpita mchezaji wa timu ya Rahaleo akiwa chini, wakati wa mchezo wao wa Bonaza Kombe la Masauni timu hizo zimetoka sare ya 2--2
Golikipa wa timu ya Rahaleo Saleh Machupa akiokoa mpira golini kwake wakati wa mchezo wao Bonaza Kombe la Masauni inayofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja Zanzibar Bonaza hilo limedhaminiwa na Mbunge wa Kikwajuni Mhe. Hamad Masauni ili kuinua vipaji vya Vijana katika mchezo wa Soka Zanzibar.
No comments:
Post a Comment