Mwenyekiti wa Makampuni ya Hoteli ya Mark and High Class Group Tanzania Rustam Merani akimuonesha moja ya vyumba cha Hoteli hiyo Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk mara baada ya kuizundua rasmi. |
Na Faki Mjaka
Maelezo Zanzibar
Upatikanaji
wa huduma bora za Kiutalii ikiwemo Hoteli za kisasa ni miongoni mwa
Vivutio muhimu vya Watalii kuja kuitembelea Zanzibar.
Hayo
yameelezwa na Waziri wa Habari,Utamaduni,Utalii na Michezo Zanzibar
,Said Ali Mbarouk katika uzinduzi wa Hoteli ijulikanayo kama TAUSI
Palace iliyopo Mji Mkongwe mjini, Zanzibar.
Amesema
Utalii imara huambatana na huduma bora na kwamba uwepo wa Tausi Palace
utasaidia ongezeko la Watalii na kupelekea kuimarika zaidi Sekta hiyo.
Waziri
Mbarouk amesema kwa sasa Sekta hiyo inaajiri zaidi ya watu Elfu 20, na
kuchangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la Pato la taifa.
Amefahamisha
kuwa Serikali itaendelea na juhudi zake za kuwahamasisha Wawekezaji
kuwekeza katika Sekta hiyo ili kuzidi kuimarisha Uchumi wa Zanzibar.
Amesema
Zanzibar ina vivutio Vingi vya Utalii na mazingira salama ya
kiuwekezaji na kuwaomba Wawekezaji hao kuendelea kutumia fursa hiyo ili
iweze kuwanufaisha wao na Jamii kwa ujumla.
Waziri
Mbarouk amesema anaamini Ubora wa Hoteli hiyo utapelekea Watalii
mbalimbali wanaofika Zanzibar kufika katika Hoteli hiyo na kujionea
Ubora wa huduma zake.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Kampuni ya Hoteli za “Mark and High Class
Group” inayomiliki Hoteli mbalimbali Zanzibar na Tanzania Bara amesema
lengo lao ni kutoa huduma bora za kiutalii ili ziwanufaishe na kuisaidia
jamii ya Zanzibar.
Amesema
Kampuni yao imevutika na Vivutio vingi vya kiutalii Zanzibar sambamba
na hali ya utulivu na amani iliyopo jambo ambalo litapelekea Sekta hiyo
kupiga hatua siku hadi siku.
Aidha amesema wapo njiani kujenga Hoteli bora ya Nyota tano katika Eneo la Mbweni ifikapo June mwakani.
Kwa
upande wake Meneja Mkuu wa Hoteli hiyo John Kiruthi amesema ubora wa
huduma zao na kujitangaza vyema katika Soko la Utalii la Dunia ndiko
kutakakopelekea kupata wageni wengi katika Hoteli hiyo.
Aidha
amesisitiza kuwa watahakikisha agizo la kuajiri Asilimia 30 ya
Wafanyakazi kutoka Zanzibar linatekelezwa ili kuisaidia Serikali
kupunguza tatizo la Ajira kwa Vijana.
Miongoni
mwa mambo ya upekee ya Hoteli hiyo ni pamoja na kuwepo kwa Vyumba
Vikubwa, Ukumbi mkubwa wa Mikutano na Wahudumu wakarimu.
No comments:
Post a Comment