Maisha/Afya : Kampeni ya Shamiri Kusomesha Watoto 112 - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


17 Jul 2015

Maisha/Afya : Kampeni ya Shamiri Kusomesha Watoto 112





Meneja Mahusiano shirika  la The Foundation For Tommorow ,Anton Asukile akifafanua jambo juu ya Kampeni ya SHAMIRI inayolenga kuchangisha milioni 50 kwa ajili ya kusaidia watoto wanaoishi kwenye
mazingira hatarishi ,kulia ni Meneja Programu wa masuala ya kijamii na afya Hedwiga na kushoto ni  Hilda Lema (Mfanyakazi).Picha na Ferdinand


Na Ferdinand Shayo wa Wazalendo 25 Blog,Arusha.
Shirika lisilo la kiserikali la The Foundation for Tommorow limezindua kampeni  ya kuchangia  SHAMIRI ya kusaidia elimu ya watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu lengo ni kuchangisha  kiasi cha shilingi
milioni 50 zitakazowawezesha kupata elimu bora na kuondokana na mazingira yanayowakabili.

Meneja Mahusiano wa shirika hilo Anton Asukile alisema hayo jana akizindua  kampeni  maalumu ya SHAMIRI   inalenga  kusaidia ustawi wa watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.

“Kampeni hii itawezesha kuinua uchumi wa kaya 40  za watoto  wanaoishi katika mazingira hatarishi  kupitia mradi wa WEZESHA KAYA pia itasaidia upatikanaji wa vifaa muhimu vya kujifunzia kwa watoto
wapatao 112” Alisema Anton

Asukile ameiomba jamii ya Watanzania kushiriki  katika kukabiliana na changamoto zinazoikabili jamii ili kuwakomboa watoto wanoishi katika mazingira hatarishi kwa kuchangia kampeni ya SHAMIRI.

Alisema kuwa Watanzania wataweza kuchangia fedha hizo kwa njia ya simu katika  kampeni hiyo imeanza rasmi mwenzi Julai na itahitimishwa septemba 25 mwaka huu.

Meneja Programu wa masuala ya kijamii na afya Hedwiga amesema kuwa
baada ya kutoa misaada kwenye familia duni wameona ni vyema wakazipatia mafunzo ya ujasiriamali na mikopo ili waweze kujikwamua na kusomesha watoto wao pasipo kutegemea misaada.

Hedwiga ameitaka jamii ya watanzania kuamka na kusaidia watoto yatima na wanaotoka kwenye familia masikini badala ya kusubiri mashirika kutoka nje yaje kutoa misaada.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad