Matukio :TANAPA yaandaa Semina ya Wajibu wa Vyombo vya Habari katika kukuza utalii jijini Mwanza - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


29 Jun 2015

Matukio :TANAPA yaandaa Semina ya Wajibu wa Vyombo vya Habari katika kukuza utalii jijini Mwanza


 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa,Ndugu Allan Kijazi akizungumza jambo,wakati wa ufunguzi wa Warsha ya Wahariri wa Habari Tanzania,mapema leo asubuhi jijini Mwanza.Ndugu Kijazi alisema kuwa Utalii ni sekta mtambuka na inachochea ukuaji wa sekta nyingine ikiwa ni pamoja na kilimo, usafirishaji wa anga na barabara, huduma za fedha, huduma za chakula na malazi kudorora kwa sekta nyinginezo.  "Hivyo kudorora kwa sekta hii huchangia kwa kiasi kikubwa kudorora kwa sekta nyingine.  Aidha, hadi sasa, Utalii unaongoza katika kuingiza fedha za kigeni ikiwa ya kwanza na kufuatiwa na sekta ya madini na kilimo.  

 Kwa  na kwa ujumla unachangia asilimia 17.5 ya Pato la Taifa lakini tathmini inaonyesha sekta hii inaweza ikachangia zaidi ya 30% ya pato la Taifa.  Asilimia zaidi ya 80 ya utalii nchini ni utalii wa kutembelea kwenye Hifadhi za Taifa, na hii inaonyesha kuwa hifadhi hizi ni muhimu kwa ustawi wa taifa letu.  Ni zaidi ya mara tatu ya idadi ya wanaotembelea Hifadhi hizi'',alisema Ndugu Kijazi.

Alisema kuwa  Maeneo yaliyo chini ya Hifadhi za Taifa yana faida nyingi za kiikolojia (ecosystem services) kama vile kuwa vyanzo vya maji (mfano; Hifadhi za Kilimanjaro, Arusha na Udzungwa). Maji hayo pia hutumiwa kwa ajili ya kuzalisha umeme unaotumika kwenye gridi ya Taifa. Hivyo faida za kusimamia Hifadhi hizi haziishii tu kwa watalii kufurahia bali pia kuna faida nyingine za kiuchumi ambazo sio rahisi sana kuziainisha katika mfumo wa kifedha (i.e. other values which are not easily tagged in financial terms).

Ndugu Kijazi alisema mwaka huu 2015, mtandao maarufu wa kimataifa unaojulikana kwa jina la Safari Bookings” uliiteua Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kuwa “The best park for African safaris” na hii ni baada ya kushindanishwa na hifadhi nyingine 50 Barani Afrika zikiwemo za Afrika Kusini.
Aidha, Hifadhi za Mikumi na Arusha zilitunukiwa “Certificate of Excellence” na mtandao maarufu duniani ujulikanao kama TripAdvisor.

Katika ufunguzi wa Warsha hiyo,Ndugu Kijazi alisema kuwa, Kauli mbiu ya Mkutano wa mwaka huu ni  “Wajibu wa Vyombo vya Habari katika kukuza utalii”. aliongeza kusema kuwa pamoja na kuelezea shughuli za TANAPA, mada zitakazowasilishwa zitahusu masuala ya Utalii na Uhifadhi na namna wanahabari wanavyoweza kushirikiana na TANAPA katika kuhimiza uhifadhi na kuendeleza utalii.  "Mada kuu nne zitawasilishwa na viongozi wa TANAPA na wanazuoni maarufu akiwemo Nd. Jenerali Ulimwengu na Dkt. Alfred Kikoti. Inatarajiwa kuwa washiriki watapata fursa ya kuchangia na mwishoni watatushauri namna ya kuboresha utekelezaji wa majukumu yetu",alisema Kijazi.
 Mkurugenzi wa Utalii na Masoko TANAPA,Bwa.Ibrahim Mussa akifafanua jambo katika Warsha ya siku tatu ya Wahariri wa Habari na Wana habari kutoka vyombo mbalimbali,inayofanyika jijini Mwanza katika hotel ya Gold Crest. Kauli mbiu ya Mkutano wa mwaka huu ni  “Wajibu wa Vyombo vya Habari katika kukuza utalii”. Pamoja na kuelezea shughuli za TANAPA,aidha imeelezwa katika Warsha hiyo kuwa mada zitakazowasilishwa zitahusu masuala ya Utalii na Uhifadhi na namna wanahabari wanavyoweza kushirikiana nasi katika kuhimiza uhifadhi na kuendeleza utalii. 
 
 Baadhi ya Wahari wa Habari kutoka vyombo mbalimbali wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri katika Warsha ya siku tatu ya Wahariri wa Habari kutoka vyombo mbalimbali,inayofanyika jijini Mwanza katika hotel ya Gold Crest. Kauli mbiu ya Mkutano wa mwaka huu ni  “Wajibu wa Vyombo vya Habari katika kukuza utalii”. Pamoja na kuelezea shughuli za TANAPA.
Meneja Uhusiano wa Shirika la Hifadhi za Taifa nchni (TANAPA),Pascal Shelutete akifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa kwenye semina hiyo mapema leo asubuhi jijini Mwanza
  Baadhi ya Wahari wa Habari kutoka vyombo mbalimbali wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri katika Warsha ya siku tatu ya Wahariri wa Habari kutoka vyombo mbalimbali,inayofanyika jijini Mwanza katika hotel ya Gold Crest. Kauli mbiu ya Mkutano wa mwaka huu ni  “Wajibu wa Vyombo vya Habari katika kukuza utalii”. Pamoja na kuelezea shughuli za TANAPA.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA),Ndugu Allan Kijazi pichani kati na Meneja Uhusiano wa Shirika la Hifadhi za Taifa nchni (TANAPA),Pascal Shelutete akizungumza jambo na
 Mkurugenzi wa Utalii na Masoko TANAPA,Bwa.Ibrahim Mussa katika Warsha ya siku tatu ya Wahariri wa Habari na Wana habari kutoka vyombo mbalimbali,inayofanyika jijini Mwanza katika hotel ya Gold Crest. Kauli mbiu ya Mkutano wa mwaka huu ni  “Wajibu wa Vyombo vya Habari katika kukuza utalii”.
Uongozi wa juu wa TANAPA wakiwa katika picha ya pamoja na Wahariri wa Habari kutoka vyombo mbalimbali.
Uongozi wa juu wa TANAPA wakiwa katika picha ya pamoja

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad