Nishati Zetu : Utengaji Kazi wa Filikunjombe Wawavutia Wananchi wake, ludewa - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


26 Apr 2015

Nishati Zetu : Utengaji Kazi wa Filikunjombe Wawavutia Wananchi wake, ludewa

Mbunge  wa Ludewa Deo Filikunjombe akishirikiana,viongozi wa CCM , wananchi na mafundi  wa mradi wa umeme kubeba nguzo za  umeme katika  kitongoji cha Ngalawale Ludewa kijijini kama  sehemu ya kuhamasisha wananchi kushiriki maendeleo
Mbunge Filikunjombe wa kwanza  kulia na katibu mwenezi wa CCM mkoa wa Njombe Honoratus Mgaya wa  kwanza  kulia wakishirikiana na mafundi wa maradi wa  umeme vijiji kuvuta kama kwa ajili ya kusimamisha nguzo ya  umeme
 mbunge Filikunjombe kulia  na diwani wa kata ya Ludewa Monica Mchilo wakifukia  nguzo ya  umeme
 wananchi na  mbunge  wakisaidiana kufukia nguzo ya  umeme
wananchi na mafundi wa  umeme  wakijiandaa kubeba  nguzo
mbunge Filikunjombe  akishiriki  kubeba  nguzo ya  umeme.
wananchi na  mbunge Filikunjombe wakiwa  wamebeba nguzo ya  umeme.
katibu  mwenezi wa CCM mkoa wa NJOMBE Honoratus Mgaya akichimba shimo la nguzo ya umeme
mbunge Filikunjombe akiwa  chini ya shimo akishiriki  kuchimba shimo la nguzo ya  umeme  kitongoji cha ngalawale  kijiji  cha ludewa wengine ni diwani wa kata ya  Ludewa MONICA MCHILO ,katibu mwenezi wa ccm mkoa wa Njombe Honoratus Mgaya na katibu mwenezi  wa CCM ludewa FELIX Haule  wakishirikiana na mbunge  wao
 mbunge Filikunjombe akitoka  katika  shimo baada ya  kumaliza  kuchimba  shimo  moja la mfano kama kuhamasisha wananchi kushiriki katika maendeleo 
........................................................................................................................................
Na MatukioDaima BLOG Ludewa
WANANCHI wa  Ngalawale kata ya Ludewa  wilaya  ya Ludewa  mkoani Njombe  wameelezwa kufurahishwa na jitihada  za  kimaendeleo  zinazofanywa na mbunge  wao Deo Filikunjombe na kukionya chama   cha  mapinduzi (CCM) katika wilaya   hiyo kutowaletea mgombea mwingine  wa ubunge  zaidi ya Filikunjombe.
Akizungumza kwa  niaba ya  wananchi wa  kata  hiyo ya Ludewa  diwani wa kata  hiyo Monica  Mchilo alisema   kuwa toka  jimbo  hilo la Ludewa kuanza kuwa na wabunge pamoja na  kuwa  kila mmoja ana jambo la  kukumbukwa ambalo amepata  kulifanya katika   jimbo hilo ila hakuna hata  mbunge  mmoja kati ya wabunge  zaidi ya  watano waliopata  kuongoza  Ludewa  ambae amepata kutekeleza ahadi zake hata robo ya ahadi  alizopata   kutoa.
Diwani Mchilo alitoa kauli   hiyo leo  wakati wa mkutano wa hadhara  wa mbunge Filikunjombe  kuwapongeza  wananchi  hao kwa kukamilisha uchimbaji  wa mashimo ya nguzo  za  umeme katika  kijiji  chao .
Alisema   kuwa wakati mbunge huyo  akiingia madarakani  mwaka 2010 moja kati ya ahadi yake ni kuhakikisha wananchi  wa  vijijini ambao  wapo pembezoni na mji  wa Ludewa  wanapatiwa  umeme na  kuwa kabla ya kumaliza  muda  wake wa ubunge tayari ahadi  hiyo  imetekelezeka na ahadi nyingine  nyingi alizopata  kuzitoa  kwa  wananchi  wa  jimbo   hilo.
Hivyo  alisema kuwa inapendeza  kuwa wana Ludewa  kuendelea kumpa muda zaidi mbunge  Filikunjombe  ili azidi  kuleta maendeleo zaidi katika  jimbo hilo badala ya kuendelea  kubadili   wabunge kila   wakati jambo  linalokwamisha maendeleo ya jimbo hilo na kuishia kuwapata   wabunge wasio na mapenzi mema na maendeleo ya wananchi.
'Ludewa  kwa  miaka  mingi   tumeteseka  kwa  kumkosa  mbunge  mwenye  uchungu  wa  maendeleo ya  wananchi  wa jimbo hilo ila  kwa mara  ya kwanza Mungu  ametupatia mbunge mwenye uchungu  wa kweli na maendeleo  yetu  hivyo lazima tumkumbatie azidi  kutawala daima'
Akielezea   kuhusu  miradi mbali mbali iliyofanyika katika  kata  yake alisema  kuwa awali umeme ulikuwepo mjini Ludewa  pekee  kwa  kipindi chote  toka  nchi ipate  uhuru  wake mwaka 1961 na  kuwa umeme  huo  aliuleta aliyekuwa  mbunge  wao stanley kolimba ambae  kwa  sasa ni mwenyekiti  wa CCM wilaya ila  kwa  kipindi cha Filikunjombe  vijiji  zaidi  vimeendelea  kupatiwa umeme na maendeleo mengine  mengi  ikiwemo  barabara ya lami Ludewa mjini.
Diwani  huyo aliwataka  wananchi  wa Ludewa kutoyumbishwa na wale wote wenye uchu wa madaraka ambao wapo kwa  maslahi yao  na badala yake  kubaki njia kuu kwa  kuendelea kuwa na mbunge  Filikunjombe kwa  kipindi kingine  zaidi.
'kwa  kuwa utaratibu wa  chama ni kutangaza uchaguzi wa  kura za maoni ila kama ingeruhusiwa tungezuia chama kutoa fomu kwa wagombea wengine wa ubunge ....lakini tunakuhakikishia wewe endelea kufanya maendeleo bila hofu kwani ni mbunge wetu wa 2015-2020 na zaidi hadi mwenyewe utakaposema basi sisi tupo na wewe'
Katibu  mwenezi  wa CCM mkoa  wa Njombe Honoratus Mgaya  alisema mbali ya kubahatika   kuwa katibu mwenezi  wa mkoa  wa Iringa uliokuwa na wilaya zaidi ya 6 na majimbo zaidi ya 10 hakupata  kuona  mbunge anayejituma  kama Filikunjombe na  kuwa mbali ya  ubunge  wake  kuwanufaisha wananchi  wa Ludewa ila bado amefanikiwa  kuutangaza  mkoa  wa Njombe na kuwa moja kati ya  wabunge wa mfano katika bunge.
Mgaya alisema  kama wabunge wote wa CCM wangeifanya kazi  ya  kuwatumikia  wananchi kama anavyofanya mbunge  huyo  wa Ludewa uwezekano wa  wapinzani kwenda bungeni ungekuwa mdogo  zaidi  na kuwa chuki ya wananchi dhidi ya CCM  ni  kutokana na baadhi ya wabunge ,madiwani na viongozi wengine wa umma kushindwa kuwajibika katika kuwatumikia wananchi .
Nae mbunge Filikunjombe akiwashukuru wananchi hao  alisema  kuwa moja kati ya ndoto  yake ni kuona wananchi  wa Ludewa wanaungana na watanzania wengine  katika kunufaika na uhuru wao kwa  kupatiwa umeme na huduma  nyingine za kijamii.
Kwani  alisema amepata  kupigania  kuona wananchi  wa vijiji 14 vya jimbo la Ludewa ambao walikuwa  gizani kwa muda  wote wa nchi ilipopata uhuru wanapatiwa umeme kabla ya kumaliza kipindi chake  cha kwanza na ubunge na kuwa kamwe hatakubali  kuona mtu yeyote anashiriki kukwamisha ndoto yake  hiyo ya  kuwaletea maendeleo wananchi .

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad