Matukio : Zanzibar Inahitaji Kuendelea kuwa Salama na Tulivu - Balozi Seif Idd - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


17 Apr 2015

Matukio : Zanzibar Inahitaji Kuendelea kuwa Salama na Tulivu - Balozi Seif Idd

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Kati Kati akishindikizwa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Said Mohd Dimwa Kulia yake mara baada ya kuhudhuria Mkutano wa pamoja  kati ya Uongozi wa Kampuni inayohusika na masuala ya Teknolojia ya Kisasa ya mawasiliano ya Baharini  { SRT } na watendaji wa sekta ya Habarini hapo Zanzibar Ocean View.
  Afisa Mkuu wa Mradi wa Teknolojia ya Kisasa ya mawasiliano ya Baharini  wa Kampuni ya { SRT } kutoka Nchini Uingereza  Bwana Simon Tucker akielezea umuhimu wa kifaa cha mawasiliano kinachotumika katika vyombo vya usafiri Majini kwenye Mkutano wa pamoja na watendaji wa Sekta ya Baharini hapa Zanzibar.
Balozi Seif akizungumza na Wanahabari   mara baada ya kuhudhuria Mkutano wa pamoja kati ya Uongozi wa Kampuni inayohusika na masuala ya Teknolojia ya Kisasa ya mawasiliano ya Baharini  { SRT } ya Nchini Uingereza na  watendaji wa Taasisi zinazohusika na sekta hiyo hapo Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Zanzibar ikiwa ni sehemu ya Dunia hii  inahitaji kuendelea kuwa salama na tulivu kutokana na mazingira yake yaliyozunguukwa na Bahari pembe zote.
Alisema mfumo wa kisasa wa mawasiliano unaotumika katika mataifa mbali mbali Duniani uliolenga zaidi katika maeneo ya bahari  yenye kutoa utajiri mkubwa kwa   asilimia 90% ya Uchumi wa Dunia unafaa kutumika ili kuondoa shaka katika udhibiti wa uvamizi wa vitendo vya kiharamia.
Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati akizungumza na Wanahabari wa Vyombo mbali mbali hapa Nchini mara baada ya kuhudhuria Mkutano wa pamoja kati ya Uongozi wa Kampuni inayohusika na masuala ya Teknolojia ya Kisasa ya mawasiliano ya Baharini  { SRT } ya Nchini Uingereza na  watendaji wa Taasisi zinazohusika na sekta hiyo hapo Zanzibar Ocean View Kilimani Mjini Zanzibar.
Alisema yapo matukio kadhaa ya uvamizi wa vyombo vya Baharini yaliyowahi kuibuka  na kuripotiwa katika ukanda wa Pembe ya Afrika ambayo yalikuwa yakitekelezwa na maharamia kutokana na udhaifu wa mawasiliano uliokuwepo wakati huo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliridhika na kukubaliana na Mfumo wa kisasa waTeknolojia ya mawasiliano ya Baharini  unaotumiwa na Kampuni ya          { SRT } ya Nchini Uingereza katika Mataifa mbali mbali Duniani ambao umesaidia kupunguza wimbi la uharamia katika maeneo ya Baharini.
Akiwasilisha mada ya mfumo wa utendaji kazi wa Kampuni hiyo kwenye  Mkutano huo Afisa Mkuu wa Mradi wa Teknolojia ya Kisasa ya mawasiliano ya Baharini  wa { SRT }  Bwana Simon Tucker alisema  kifaa maalum cha Mawasiliano huwekwa kwenye chombo cha Baharini ambacho husaidia kutoa taarifa za mawasiliano.
Bw. Simon alisema chombo hicho kidogo kinachoweza kuwekwa kwenye boti au hata meli za uvuvi na abiria kinauwezo wa kusafirisha mawimbi ya mawasiliano kwa zidi ya meli 40.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad