Matukio : WaTanzania Waliokwama Afrika Kusini Warejea Nyumbani - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


26 Apr 2015

Matukio : WaTanzania Waliokwama Afrika Kusini Warejea Nyumbani



JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA


Coat of Arms
 

Simu: 255-22-2114615, 211906-12
Barua pepe: nje@nje.go.tz
Barua pepe: gcu@nje.go.tz

Nukushi: 255-22-2116600

              

 


                20 KIVUKONI FRONT,
                           P.O. BOX 9000,
                  11466 DAR ES SALAAM, 
                                    Tanzania.

 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
WATANZANIA WALIOKUWA AFRIKA KUSINI WAMEREJEA NYUMBANI
Kundi la Watanzania 26 limerejea nyumbani kutoka Afrika Kusini  leo tarehe 26 Aprili, 2015 kufuatia mashambulizi ya wazawa dhidi ya wageni.  Kundi hilo la kwanza kurejea nyumbani liliwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere saa 11 alfajiri na Ndege ya Fast Jet. 

Watanzania hao walikuwa wanaishi katika kambi za dharura za Isipingo na Phoenix zilizopo jijini Durban. Walisindikizwa kurudi nyumbani na  Afisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Bw. Elibahati Lowassa. Zoezi la kuwarejesha wananchi hao lilisimamiwa na kuratibiwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini. 

Wakati huo huo, Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini umepata taarifa kuwa kuna Watanzania wengine wapatao 20 wanaishi kwenye Kambi ya Hillbrough jijini Johannesburg. Ubalozi umetuma Afisa kwenda katika kambi hiyo ili kufanya uhakiki wa taarifa hizo kwa madhumuni ya kuwarejesha nyumbani Tanzania haraka iwezekanavyo.
MWISHO.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
25 Aprili 2015

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad