Mifuko ya Jamii : ECASSA Yaikutanisha Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya Nchi za Afrika Mashariki na Kati - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


27 Mar 2015

Mifuko ya Jamii : ECASSA Yaikutanisha Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya Nchi za Afrika Mashariki na Kati


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NSSF Tanzania, Abubakar Rajab, akitoa mada katika warsha juu ya uendeshaji wa bodi za mifuko ya hifadhi ya jamii iliyoandaliwa na Taasisi ya Hifadhi ya Jamii ya Africa Mashariki na Kati (ECASSA)  inayoendelea nchini Mauritius.
Wajumbe wa warsha juu ya uendeshaji wa bodi za mifuko ya hifadhi ya jamii kutoka nchi za Tanzania, Kenya, Burundi, Rwanda, Zambia, Uganda na wenyeji Mauritius wakiwa katika picha ya pamoja na Mh. Fazila Jeewa waziri wa masuala ya hifadhi ya jamii nchini Mauritius mara baada ya ufunguzi wa warsha hiyo iliyoandaliwa na taasisi ya hifadhi ya jamii ya Africa mashariki na kati (ECASSA) juu ya uendeshaji wa bodi za mifuko ya hifadhi ya jamii inayoendelea huko nchini Mauritius.
Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF (kushoto), akibadilishana mawazo na baadhi ya washiriki wa warsha hiyo.
Katibu Mkuu wa Taasisi ya Hifadhi ya Jamii ya Africa Mashariki na Kati (ECASSA) Dk. Frederic Ntimarubusa akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi ambaye ni Waziri wa Masuala ya Hifadhi ya Jamii nchini Mauritius, Fazila Jeewa kufungua warsha inayoendelea nchini Mauritius.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad