Maisha na Afya Yetu :Utafiti unaonyesha kuwa magonjwa mengi na ajali yanachangiwa na matumizi ya pombe - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


26 Mar 2015

Maisha na Afya Yetu :Utafiti unaonyesha kuwa magonjwa mengi na ajali yanachangiwa na matumizi ya pombe


Na Chalila Kibuda,
Utafiti unaonyesha kuwa magonjwa ya kifua Kikuu , Ukimwi ,Kansa pamoja na ajali zinachangiwa na matumizi ya pombe kwa kiwango cha juu, na vijana ndio waathirika wakubwa kutokana na kutokuwepo kwa sera ya matumizi ya pombe.

Utafiti huo umetolewa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu –Kituo cha Mwanza (NIMR),uliofanywa katika Mikoa ya Kilimanjaro na Mwanza na ambao ulilenga vijana kuanzia Miaka 15-24.

Wakizungumza katika semina ya wadau wa masula ya afya leo jijini Dar es Salaam ,Watafiti wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu –Kituo cha Mwanza (NIMR) , wamesema kuwa matumizi ya pombe nchini yako katika kiwango cha juu na kusababisha magonjwa kuchangiwa na matumizi hayo.

Mtafiti wa Sayansi ya Jamii wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu –Kituo cha Mwanza (NIMR), DK. Haika Osaki amesema katika utafiti wa pombe zilizo kwenye mifuko (Viroba) zinanyweka kwa kiwango cha juu na watumiaji ni vijana ambao ndio waathirika wakubwa wa magonjwa kutokana na kutumia pombe.

Haika amesema nchi ambazo zinafanana kiuchumi na Tanzania kama Zambia na Malawi wamepiga marufuku uzalishaji wa pombe za Viroba kutokana na kuona madhara ya matumizi ya pombe hiyo ambapo vijana wengi wameona ni pombe zenye urahisi wa bei pamoja na uhifadhi wake.

Naye Mtafiti wa NIMR Mwanza, Dk. Said Kapiga amesema kuwa wamefanya utafiti na kuona madhara ya pombe na ongezeko la wagonjwa ambao wanatokana na matumizi ya pombe pamoja na mabadiliko mengine ya kimaisha.
Mtafiti wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu-Kituo cha Mwanza (NIMR), Dk. Said Kapiga akifafanua jambo wakati akitoa mada yake ya ufatiti wa Pombe,katika semina ya Wadau iliyofanyika  jijini Dar es Salaam.
Mtafiti wa Sayansi ya Jamii wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu –Kituo cha Mwanza (NIMR) ,DK. Haika Osaki akitoa maada juu matumizi ya Pombe za Viroba katika semina ya wadau iliyofanyika  jijini Dar es Salaam.
Mshauri wa masuaya Afya na Familia, Dk. Ali Nzige akitoa mada katika semina ya wadau juu madhara ya pombe,kwenye semina iliyofanyika  Jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wadau wakifatilia maada za utafiti wa pombe katika mkutano uliofanywa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu-Kituo cha Mwanza (NIMR) iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mtafiti wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu-Kituo cha Mwanza (NIMR), Dk. Said Kapiga akizungumza ma waandishi wa habari juu ya utafiti wa pombe nchini, wakati wa semina iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Kudhibiti Tumbaku nchini ,Dk.Lutgard Kokulinda Kagaruki akizngumza na waandishi wa habari juu ya madhara ya Pombe katika semina ya wadau iliyofanyika  jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad