Matukio : Gwajima Atakiwa kuhojiwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za Kashfa na Matusi dhidi ya Kardinali Pengo - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


26 Mar 2015

Matukio : Gwajima Atakiwa kuhojiwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za Kashfa na Matusi dhidi ya Kardinali Pengo


Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamtaka Askofu JOSEPHAT GWAJIMA wa Kanisa la Ufufuo na Uzima afike haraka katika kituo cha Polisi cha Kati ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa mahojiano kuhusu tuhuma za kashfa na matusi.

JAMHURI YAA MUUNGANO WA TANZANIÀ
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
PRESS RELEASE
26/03/2015
ASKOFU GWAJIMA ATAKIWA KUHOJIWA NA JESHI LA POLISI KUHUSU TUHUMA ZA KASHFA NA MATUSI DHIDI YA KALDINARI PENGO.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamtaka Askofu JOSEPHAT GWAJIMA wa Kanisa la Ufufuo na Uzima afike haraka katika kituo cha Polisi cha Kati ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa mahojiano kuhusu tuhuma za  kashfa na matusi.
Tumepokea malalamiko ya kukashifiwa na kutukanwa hadharani Mwadhama Kaldinari Polycarp Pengo ambaye ni kiongozi wa Kanisa Katoliki nchini Tanzania. Kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii kama vile WhatsApp na mingineyo kuna sauti iliyorekodiwa (audio) na picha za video (Video Clip) zikimuonyesha Askofu Gwajima akimkashfu na kumtukana kwa maneno makali Kaldinari Pengo katika hali ambayo pia imewaudhi watu wengine.
Baada ya tukio hilo juhudi mbalimbali zimekuwa zikifanyika katika hali ya kawaida ili kumpata Askofu Gwajima bila mafanikio na hivyo yeye mwenyewe sasa anatakiwa aende akaripoti haraka kwa Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam bila kukosa.
Ni muhimu sana kwa Askofu Josephat Gwajima kuripoti yeye mwenyewe badala ya Kutafutwa au kukamatwa ili ajibu tuhuma hizo kutokana na nafasi yake katika jamii.
Jalada la uchunguzi limefunguliwa na upelelezi wa shauri hili unaendelea ili sheria. ichukue mkondo wake.
S. H. KOVA,
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad