Na Mwandishi wetu
Bodi
ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) imepokea ugeni wa wanachuo
sabini wa mwaka wa pili wanaosoma stashahada ya ununuzi na ugavi
waliokuja kwenye ziara ya mafunzo kutoka Chuo cha Utumishi wa Umma tawi
la Tanga.
Ziara hiyo ya mafunzo ililenga kujua kazi mbalimbali za Bodi ya wataalam wa ununuzi na Ugavi (PSPTB).
Mkurugenzi mkuu Mtendaji wa PSPTB Dr Clemence Tesha, aliupokea
ugeni huo, na kuwashukuru kwa kuona nia ya kufanya ziara ya mafunzo.
Aidha aliwaelezea umuhimu wa kuzingatia maadili , kujifunza kwa bidii
ili kupata maarifa na ujuzi unaoweza kuhimili soko la ushindani la ajira
.
Wanachuo
pia walielezewa juu ya taratibu za mitihani ya Bodi yenye ngazi ya
cheti cha awaliAwali, msingi Msingi na Taaluma. Aidha aliwaelezea
taratibu za kusajii kwa ajili ya kufanya mitihani ya kitaaluma mara
baada ya kumaliza masomo yao na kwamba mhitimu wa stashahada ya ununuzi
na ugavi kwa chuo kinachotambuliwa na Bodi anaanzia ngazi ya kwanza ya
mitihani ya taaluma.
Mitihani ya taaluma ina ngazi tano, ambazo huhitimishwa kwa wanafunzi kufanya mitihaniutafiti.
Ziara hiyo pia ilitoa fursa kwa wanachuo hao kujua taratibu za
kujisajili kama wataalum wataalam wa Ununuzi na Ugavi kwani ni hitaji la
sheria iliyounda Bodi.
Aidha walifahamishawa kwamba kuna ngazi mbalimbali za usajili ambazo zinatambua kiwango cha ujuzi na uzoefu wa mtaalam.
“ fanyeni usajili mara mmalizapo chuo ili kutumia fursa za ajira katika fani yenu “ ” alisisitiza.
Tambueni kwamba taaluma ya ununuzi na ugavi inaongozwa na misingi ya
maadili ambayo inawataka kutambua kuwa mnawajibika kwa umma wa
watanzania, taaluama yenu, mwajili wako. Misingi hii ya wajibu ndio
inayoifanya taaluma hii iwe ya kipekee. “maadili huanzia.
Wageni wakiwasili kwenye ofisi za Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi.
Mkurugenzi
Mtendaji Mkuu wa PSPTB, Dr Tesha akitoa hutuba ya ufunguzi
kuwakaribisha wanachuo wa mwaka wa pili wa stashahada ya Ununuzi na
Ugavi kutoka chuo cha TPSC Utumishi wa Umma tawi la Tanga.
Wanachuo wakimsiliza Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Bodi Dr. Tesha.
Mkurugenzi ya Mafunzo, Bw. Godfred Mbanyi akielezea juu ya madaraja ya mitihani ya Bodi na taratibu za kufanya mitihani.
Bw.
Ally Songoro kutoka Kurugenzi ya Taaluma akifafanua jambo, juu ya
taratibu za usajili, miiko ya wanataaluma kwa wanachuo waliotembelea
Bodi.
Bw. Paul Bilabaye kutoka Kurugenzi ya Fedha na Utawala akielezea taratibu za malipo ya huduma mbalimbili zitolewazo na Bodi.
Mwanachuo mmoja akiuluza maswali juu ya kazi mbalimbali za Bodi Wataalam wa Ununuzi na Ugavi.
Mmoja wa wanachuo akiuliza maswali juu ya kazi mbalimbali za Bodi Wataalam wa Ununuzi na Ugavi.
Wanachuo wakiwa kwenye picha ya pamoja kwenye ofisi za Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi.
Baadhi
ya wanafunzi kwenye picha ya pomoja pamoja na mkurugenzi Mkurugenzi
mtendaji wa Bodi Dr. Clemence Tesha na viongozi waandamizi wa Bodi.
No comments:
Post a Comment