Mkuu
wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam (CBE) Prof. Emanuel Mjema
akizungumza wakati wa mkutano wa wadau na wataalam wa elimu kutoka
Taasisi za Elimu, vyuo, walimu wa masomo ya Biashara wa shule za
Sekondari waliokutana kupitia Mtaala wa kufundishia mafunzo ya taaluma
ya Ualimu katika Biashara jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi
wa Mafunzo ya awali wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Dkt. Esther
Mbise akitoa ufafanuzi kwa wadau wa Elimu kuhusu uandaaji wa mtaala wa
kufundishia walimu wa masomo ya Biashara jijini Dar es salaam.
Menejimenti
na watendaji wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) wakiwa katika picha ya
pamoja mara baada ya kufunguliwa kwa mkutano wa wadau na wataalam wa
elimu kutoka Taasisi za Elimu, vyuo, walimu wa masomo ya Biashara wa
shule za Sekondari na vyuo na wadau mbalimbali wa Elimu jijini Dar
es salaam.
Na. Aron Msigwa.
Chuo
cha Elimu ya Biashara Kampasi ya Dar Es salaam (CBE) kwa kushirikiana na
wadau mbalimbali wa elimu nchini kiko katika hatua za mwisho za
kukamilisha Mtaala wa kufundishia Walimu wa masomo ya biashara kwa ngazi
ya shahada utakaoanza kutumika katika mwaka masomo utakaoanzia mwezi
Septemba 2015.
Akizungumza
wakati wa mkutano wa wadau na wataalam wa elimu kutoka Taasisi za
Elimu, vyuo, walimu wa masomo ya Biashara wa shule za Sekondari na vyuo
na wadau mbalimbali wa Elimu leo jijini Dar es salaam, Mkuu wa chuo
hicho Prof. Emanuel Mjema amesema chuo chake kimeamua kuanzisha programu
hiyo ili kuziba pengo la uhaba wa walimu wa kufundisha masomo ya
Biashara wenye taaluma ya ualimu.
Amesema
chuo hicho kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kimefikia uamuzi huo
kufuatia utafiti uliofanywa na jopo la wataalamu wa maandalizi ya
Mtaala huo kuanzia mwaka 2012 uliobaini uwepo wa kiwango kikubwa cha
uhitaji wa waataalam wa kufundisha masomo ya biashara wenye taaluma ya
ualimu.
Prof.
Mjema amesema katika utafiti huo ilibainika kuwa asilimia 27 ya walimu
wanaofundisha masomo ya Biashara katika maeneo mbalimbali nchini wana
taaluma ya ualimu huku asilimia 73 wanafundisha kwa kutumia uzoefu jambo
linalochangia kupungua kwa ubora wa ufundishaji darasani.
“Sisi
kama chuo cha Elimu ya Biashara tumeona uhitaji uliopo nchini wa kukosa
wataalam wa kufundisha masomo ya Biashara wenye taaaluma ya ualimu ndio
maana tumeamua kuanzisha mtaala huu wa kufundishia wanafunzi wa Shahada
ya Elimu katika Biashara ili tupate wahitimu bora watakaofundisha
wanafunzi wetu na kukidhi mahitaji ya soko” Amesisitiza.
Amesema
mafunzo yatakayotolewa yatachukua muda wa miaka 3 na kubainisha kuwa
katika mahafali ya kwanza ya shahada hiyo wanafunzi wapatao 300
wanatarajia kuhitimu mafunzo hayo.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Mafunzo ya awali wa Chuo cha Elimu ya Biashara
(CBE) Dkt. Esther Mbise akitoa ufafanuzi kuhusu uandaaji wa mtaala huo
amesema timu ya wataalam wa maandalizi ya mtaala huo ilikutana na wadau
mbalimbali kutoka Wizara ya Elimu,Taasisi za elimu, wanafunzi, wazazi na
Taasisi za Mitaala ya Elimu ili kupata maoni yao na kupata maoni
yaliyoanisha maeneo ya kufanyia marekebisho ili kuwa na mtaala bora
wenye kukidhi mahitaji ya elimu ya biashara nchini.
Naye
Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya mtaala huo ambaye pia ni Mkuu wa
Idara ya Masoko wa CBE akiwasilisha mtaala huo ili upitiwe na wadau
wadau waliohudhuria mkutano huo amesema sababu za kuwepo kwa mabadiliko
ya kuwepo kwa mtaala huo ni kuwepo kwa mahitaji ya wataalam wa
kufundisha masomo ya Biashara wenye taaluma ya Ualimu.
Amesema
mtaala huo utakaoanza kutumiwa mwezi Septemba, 2015 utatoa fursa ya
wanafunzi wengi zaidi waliohitimu kidato cha sita na vyuo kujiunga
katika masomo hayo ya miaka 3 ya Shahada ya Elimu katika biashara.
No comments:
Post a Comment