Teknolojia na Biashara : OBI Kuwekeza Kwenye Soko la SMARTPHONE Zenye Gharama Nafuu Tanzania - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


23 Jan 2015

Teknolojia na Biashara : OBI Kuwekeza Kwenye Soko la SMARTPHONE Zenye Gharama Nafuu Tanzania


DSC_0248
Mkurugenzi Mtendaji wa Obi Mobiles, Afrika Mashariki na Kati na Afrika, Amit Rupchandani (katikati) akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari )hawapo pichani) jijini Dar leo wakati wa utambulisho wa simu za aina ya smartphone zinazotengenezwa na Obi. Kushoto ni Mkurugenzi wa DESPEC Afrika, Farouk Jivani ambao ndio wasambazaji wakuu wa bidhaa hizo Tanzania na Afrika Mashariki na Kulia Mkuu wa kitengo cha masoko na mawasiliano wa Obi, Yusuf Khan.(Picha na Zainul Mzige).
Na Andrew Chale
Kampuni mpya ya simu za Smartphone ya Obi Mobiles imezindua bidhaa zake katika soko la Tanzania pamoja na Nchi za Afrika Mashariki, kwa ubia na kampuni ya DESPEC wasambazaji wanaoongoza katika soko la usambazaji wa bidhaa za IT.
Wakizungumza na wandishi wa habari leo katika Hotel ya Serena, jijini Dar es Salaam, wakati wa utambulisho rasmi wa kampuni hiyo ya simu ya Obi iliyoanzishwa na mtaalam wa masoko na Mkurugenzi wa zamani wa kampuni ya Apple, John Sculley, Akizumgumza kwa niaba ya Sculley. Mkurugenzi Mtendaji wa Obi Mobiles, Afrika Mashariki na Kati na Afrika, Amit Rupchandani
Alisema kampuni hiyo kwa kushirikiana na DESPEC, Obi inategemea kuanza kusambaza bidhaa zake zenye ubora zaidi katika robo ya kwanza ya mwaka huku ikitarajia kuweza kukamata soko la Tanzania kwa asilimia tano (5%) ifikapo mwisho mwa mwaka huu.
DSC_0235
Mkurugenzi wa DESPEC Afrika, Farouk Jivani (kushoto) ambao ndio wasambazaji wakuu wa bidhaa hizo Tanzania na Afrika Mashariki, akitolea ufafanuzi wa kituo cha huduma (services centre) ya simu hizo za Obi zitakazokuwa zikishughulikiwa hapa hapa nchini.
“Nia yetu ni kutumia Obi kwenye kila soko jipya ili kutengeneza bidhaa inayokubalika Kimataifa na hasa kwenye sehemu ambazo matumizi ya Smartphone yapo juu” alisema Amit Rupchandani.
Aliongeza kuwa, Katika uzinduzi uliofanyika India na Mashariki ya Kati, umeweza kuleta mafanikio makubwa kuliko walivyotegemea hivyo Obi imejiandaa na kuwekeza nguvu kupanua wigo wa biashara zake pia kwa soko la Tanzania.
Aidha, akielezea namna walivyojiandaa kushika soko la Afrika, Amit Rupchandani alisema soko la Afrika lina nafasi kubwa kwenye bidhaa za smartphone kutokana na ongezeko kubwa katika matumizi ya Teknologia na hasa miongoni mwa vijana.
DSC_0307
Mkurugenzi wa DESPEC Afrika, Farouk Jivani (kushoto) ambao ndio wasambazaji wakuu wa bidhaa hizo Tanzania na Afrika Mashariki, akionyesha aina moja ya simu za Obi ambazo zitakuwa na garantii ya mwaka mmoja na miezi minne.
“Wateja wanataka kutumia Smartphone zilizo nzuri zenye bei nafuu bila kuathiri ubora wake. Pia kuna ongezeko la matumizi ya Iphone ukilinganisha na Smartphone. Utafiti wetu umeonesha ya kwamba wateja wanaweza kubadilisha matumizi ya bidhaa yeyote ilmradi wana imani nayo, hivyo Obi imejiandaa kukabiliana na hilo na hakika watazifurahia”. Alisema
Aidha, Amit Rupchandani alibainisha kuwa, licha ya soko la bidhaa za simu za mkononi kuwa bidhaa za bei kubwa, wao hawatakuwa hivyo kwani lengo lao ni kuongeza watumiaji wa simu za mkononi ambao wangependa kutumia smartphone zenye ubora bila kuingia gharama kubwa.
“Falsafa yetu ya ‘Kama ulivyo’ inamaanisha Obi haibagui, inakuwezesha ulivyo ambapo tuna bidhaa mbalimbali kwa watu wa aina tofauti”. alimalizia Amit Rupchandani.
DSC_0313
Mkuu wa kitengo cha masoko na mawasiliano wa Obi, Yusuf Khan (kulia) akionyesha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) application mbalimbali zinazopatikana kwenye simu hizo.
Kwa upande wake, Mkurugezi wa DESPEC Afrika, Farouk Jivani alisema kampuni yake inayo furaha kuwa msambazaji wa kipekee wa bidhaa za Obi Mobiles Tanzania na Afrika Mashariki kwani wamejidhatiti kuhakikisha zinawafikia watumiaji sokoni.
“Kuingia kwa kwa bidhaa za Obi Mobiles sokoni kunaashiria ongezeko la matumizi ya simu za mkononi na pia matumizi ya intaneti, hivyo tunafanya juhudi kuhakikisha Obi inatengeneza jina la kudumu kwa bidhaa zake katika hili” alisema Farouk Jivani.
Obi Smartphone kwa soko la Afrika, inatarajiwa kuziduliwa mwezi Machi mwaka huu hapa Nchini ikifuatiwa na Nchi zingine za Afrika.
DSC_0318
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakikagua ubora wa simu za Obi.
DSC_0323
Kipeperushi kikionyesha aina mbalimbali za simu za smartphone za kampuni ya Obi zitakazokuwa zikiuzwa kuanzia shilingi 120,000 mpaka 340,000.
DSC_0325

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad