Mizengwe Kwenye Riadha :Athletics Intelligence: Nyambui akiri kupokea hongo na kugushi sahihi - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


11 Dec 2014

Mizengwe Kwenye Riadha :Athletics Intelligence: Nyambui akiri kupokea hongo na kugushi sahihi


 
Chama Cha Riadha kilikaa kikao tarehe 6 December 2014 mjini Dar Es Salaam, kikao hicho kilichoelezewa kuwa kikali kuwahi kupata kutokea katika hitoria ya chama hicho kilimweka Katibu wa RT Suleiman Nyambui kiti moto hadi akafanya jaribio la kutaka kukimbia ukumbini.


Baada ya shutuma nyingi, zote zikielekezwa kwa Nyambui na wajumbe wote wa RT hatimaye mzee akakiri huku akitetemeka kwamba: 


-         -  Alipokea hongo ya Tsh: 500,000 kutoka kwa wanariadha waliokwenda mazoezi kambi za nje.


-        -  Ndiyo maana hakuruhusu utaratibu wa mchujo kwanza ili awapange wale waliokubali kumlipa.


-        - Pia amekiri kuendesha semina zisizotambuliwa na RT na kuguhi sahihi zilizopo kwenye vyeti.


-       -Amekiri yote hayo baada ya baadhi ya wajumbe kutishia kuweka wazi ushahidi walionao.


KUMBUKUMBU: Watanzania wakumbuke kwamba kupitia blog hii tumeshawahi kumtahadharisha Waziri Membe kuwa makini na fedha za walipa kodi. Sasa unaona mhehimiwa Waziri? Fedha ulizotoa kwa moyo wa kizalendo imekuwa chanzo cha ufisadi wa ndani ya RT!


Pia Nyambui alikaririwa na chombo kimoja maarufu cha habari hapa nchini mwezi July mwaka huu akikiri kwamba “Aliwahi kuwasafirisha watu ambao walibainika kubeba madawa ya kulevya hadi Australia” Je Nyambui anaendelea kufanya nini RT?

Muda si mrefu ‘Athletics Intelligence’ tutatoa ushahidi wa video ambao utamuumbua Nyambui pamoja na familia yake maana hakika NYAMBUI AMEZIDI. 
Chanzo : www.gidabuday.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad