Matukio : Mhe. Joshua Nassari Aachiwa kwa Dhamana baada ya tuhuma za Kuchoma Bendera ya CCM na Kutishia kwa Silaha - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


17 Dec 2014

Matukio : Mhe. Joshua Nassari Aachiwa kwa Dhamana baada ya tuhuma za Kuchoma Bendera ya CCM na Kutishia kwa Silaha

Na Woinde Shizza

Hakimu David Mwita wa Mahakama ya mwanzo ya maji ya chai ameahirisha hadi disemba 24, shauri la kesi inayomkabili Mbunge wa Jimbo la Arumeru mashariki Joshua Nassari (CHADEMA), kwa tuhuma za kuharibu mali ya uma kwa kuichoma Bendera ya CCM ,yenye dhamani ya shilingi laki mbili pamoja na kumteka mtu na kumtishia kwa bunduki tukio ambalo anatuhumiwa kufanya Disemba15 mwaka huu.

mahakama hiyo imeweza kumuachia mbunge huyo mara baada ya kutimiza mashariti ambapo shariti la kwanza ni kuwa na wathamini wa tatu ambao wanamali zisizo amishika zenye dhamani ya shilingi milioni moja na nusu kila mmoja.

Katika kesi hiyo inayomkabili mbunge huyo ambayo mlalamikaji wa kesi hiyo akiwa ni mtu binafsi hakimu wa kesi hiyo mara baada ya kusikiliza mashitaka hayo alichukuwa nafasi ya kuhairisha kesi hiyo adi december 24 ambapo kesi hiyo itatajwa tena kwa mara nyingine.

Akiongea mara baada ya kuairisha kesi hiyo wakili wa mbunge huyo wa Arumeru mashariki James Ole milya alisema kuwa amesikitishwa sana na tukio la mahakama hiyo kumpa mashariti makubwa mteja wake kwani kesi yake ilikuwa haitaji mashariti makubwa hivyo .

Aidha alisema kuwa mbali na kupewa mashariti hayo angependa kesi hiyo ipelekwe katika mahakama ya wilaya ili yeye kama wakili wa mbunge huyo aweze kumtetea kwani katika mahakama ya mwanzo hairuhuu kuweka wakili.

“unajua kwakweli mbali na hivyo pamoja kuwa sio jamuhuri imemshitaki mh Nasari bali ni mtu binafsi lakini nasikitika sana kwa mashariti ambayo wameweka ,kwani ata bila ao wathamini watatu wakiwa na kitu kisichoamishikika chenye dhamani ya shilingi milioni moja na nusu,huyu ni mbunge ambapo angeweza kujidhamini ata yeye mwenyewe kwani mtu huyu ni kioo cha jamii na awezi kukimbia sehemu yoyote kwanini wasinge mpa mdhamana mapema mpaka apate wadhamini hawa na mashariti haya”alisema Milya

Aidha alisema kuwa anashangazwa sana na maamuzi haya kwani kuna mtu ambaye amemzalilisha mwanamke ambaye alikuwepo mahakamani hapo na akamvua mwanamke huyo nguo lakini yeye alishangazwa sana kwa mtuhumiwa wa kosa ilo la uzalilishaji yeye kupewa mashariti mapesi ya kuwa na mdhamini mmoja na kutoa laki tano laikini mbunge yeye amepewa mashariti ya kuwa na wadhamini watatu ambao wanamalizi zenye dhamani ya shilingi milioni moja na nusu uku akitilia shaka kuwa katika kesi hii wanahisi kuna chama cha siasa kinachangia kuongeza nguvu.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad