Happy Birthday to Me : Heri ya Siku ya Kuzaliwa Kwa CEO wa Wazalendo 25 Blog ;Gadiola Emanuel - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


25 Dec 2014

Happy Birthday to Me : Heri ya Siku ya Kuzaliwa Kwa CEO wa Wazalendo 25 Blog ;Gadiola Emanuel

Nakushukuru sana Mungu kwa Kunifikisha siku ya Leo. Nakushukuru Mama yangu mzazi kwa kunizaa , kunilea na kunitunza (japo Umepumzika ila bado nakumbuka Maonyo yako siku zote za maisha yangu ). Nakushukuru Mke wangu kipenzi Upendo Gadiel na Mwanangu kipenzi Glory Gadiel kwa Kuwa nami katika changamoto zote za Maisha yangu, ki ukweli nawapenda Sana. Nawashukuru Ndugu, Jamaa na Marafiki kwa kuwa nami bega kwa bega katika hali zote, salute to you guys.... Mwisho Nawatakia Krismasi Njema na Mwaka mpya wa 2015. Ni mimi Gadiola Emanuel Mkurugenzi wa Wazalendo 25 Blog , www.arushapublicity.com na www.northernshotstz.com . Love you All...!!!
Gadiola Emanuel the Director of Northern Shots
Gadiola Emanuel The Director of Arusha Publicity...
  Maktaba Yetu :Mablogger, wakiwa makini kunasa kila kinachozungumzwa.
Maktaba  Yetu: Jeff Msangi, akichangia mada. Kulia ni Mwenyekiti wa Arusha Bloggers Network Bw. Gadiola Emanuel na kushoto ni Shamim Mwasha wa 8020 FASHIONS Blog.
Maktaba Yetu
Woinde Shizza na Gadiola Emanuel na mapoooz. Wadau hawa waliokutana ni sehemu ndogo tu ya Bloga wa Arusha ambao hawakuweza kuhudhuria.
Ikiwa teknolojia ya mawasiliano kwa njia ya mtandano inazidi kukua na kupata umaarufu miongoni wa watanzania, wadau wa uliongo huo kwa Mkoa wa Arusha wameamua kuanzisha umoja wao ambao utalenga kuwatambulisha mbele ya jamii na mamlaka za nchi sambamba na kuongezeana ujuzi katika kuiboresha zaidi.

Mkoa wa Dar es Salaam unaonekana kuwa na wadau wengi zaidi. Mikoa mingine wapo pia, ikiwamo Arusha lakini hawafahamiki sana kitaifa kama ilivyo maeneo mengine. Kwa kutambulika na mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA, teknolojia hii inapaswa kuenziwa na kusimamiwa vyema ili jamii iweze kunufaika nayo vizuri, na wahusika nao wakinufaika kwa namna moja au nyingine.

Teknolojia hii katika uwanja wa mawasiliano inahusisha pia mitandao mingine ya kijamii kama Facebook, Tweeter n.k bila kusahahu wavuti za makampuni ama watu binafsi.

Baadhi ya maBlogga wa Jijini Arusha waliokutana katika kikao cha kujadili mustakabali wa ushiriki wao katika dunia ya utandawazi hasa katika matumizi ya mitandao ya kijamii, lengo la kukutana kwao ikiwa ni kupanga mikakati ya kuanzisha umoja wa blogga wote wanaoishi ama kufanya shughuli zao Jijini hapa.

Kutoka kushoto, majina yao na anuani za blog kwenye mabano ni Woinde Shizza kutoka LIBENEKE LA KASKAZINI (http://woindeshizza.blogspot.com; Thomas wa JITAMBUE KWANZA BLOG (http://jitambuekwanza.blogspot.com/); Gadiola Emmanuel wa WAZALENDO25 (http://wazalendo25.blogspot.com/); (Victor Machota wa ASILI YETU TANZANIA (http://victormachota.blogspot.com) na Bertha Mollel wa BERTHA BLOG (http://berthamollel.blogspot.com/). Bloga mwingine ambaye haonekani pichanni ni Seria Tumainiel wa NOISE OF SILENCE (http://arusha255.blogspot.com)

SeriaJr wa Arusha255 (mwenye sweta) akifurahia jambo na wajumbe wengine

Umakini katika kusikiliza mjadala na maoni ya wengine

Bertha Mollel na Victor Machota wakibadilishana mawazo baada ya kikao kumalizika.
Maktaba Yetu :Picha ya pamoja mara baada ya kumaliza Semina, kutoka kushoto ni Julius Felix (TCRA) , Seria Tumainiel ( Arusha 255 Blog ), Bw. Innocent Mungy (TCRA) ,Victor Machota (ASILI YETU TANZANIA Blog) ,Gadiola Emanuel (WAZALENDO 25 BLOG) na Woinde Shizza (LIBENEKE LA KASKAZINI).


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad